May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

CCM waitaka Serikali itoe ufumbuzi kupanda kwa bei ya mafuta

Spread the love

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimeitaka Serikali kutafuta ufumbuzi wa haraka wa namna ya kukabiliana hali ngumu ya maisha kwa Watanzania kutokana na kupanda kwa bei ya mafuta duniani ili kuwapunguzia wananchi makali ya maisha. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Taarifa iliyotolewa leo tarehe 9 Mei, 2022 na Katibu wa NEC ya CCM Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka imesema chama hicho kimetoa maagizo hayo kwa kuwa kimeguswa na hali hiyo ya maisha iliyopo nchini.

“Tunafanya hivyo ikiwa ni utekelezaji wa ahadi zetu kupitia ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025 ambayo tuliahidi kuisimamia serikali ili kuwaletea maendeleo Watanzania na kuimarisha ustawi wao.

“Pamoja na sababu za kitaalamu zinazotajwa kusababisha kupanda kwa bei ya mafuta na kupelekea mfumuko huu wa bei nchini, chama makini na serikali inayojali watu wake haiwezi kukaa kimya na kukosa hatua za kuchukua hatua ili kuwapunguzia mzigo wananchi,” amesema.

Amesema kutokana na hali hiyo CCM kimeitaka serikali kukaa na kuchukua hatua haraka ili kuwapa nafuu ya maisha wananchi.

Aidha, CCM kimewaomba Watanzania kuwa watulivu na kuendelea kuiamini serikali ya CCM ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan wakati huu ambao inaendelea kuchukua hatua stahiki za kupunguza makali hayo bila kuathiri shughuli zingine za maendeleo ikiwemo utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo.

error: Content is protected !!