Sunday , 28 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Blinken: NATO ipo tayari kama mzozo utatugusa
Kimataifa

Blinken: NATO ipo tayari kama mzozo utatugusa

Spread the love

 

KATIBU Mkuu wa Umoja wa Kujihami-NATO, Jens Stoltenberg, amekutana na Katibu Mkuu wa Marekani, Antony Blinken pamoja na mawaziri wa mambo ya nje wa wanachama wa umoja huo Brussels nchini Ubelgiji, kwa lengo la kujadili hatua za kuchukua juu ya uvamizi wa Urusi nchini Ukreini. Inaripoti ABC News … (endelea).

Katika mkutano na waandishi wa habari kabla mkutano huo, Blinken na Stoltenberg alilaani mashambulizi yanayofanywa na Urusi kwa raia wa Ukreini na kutoa maoni juu ya ripoti ya mashambulizi katika mitambo ya nishati ya nyuklia.

“Hii ni ishara tu ya vita ya kizembe na umuhimu wa kuhakikisha inakoma na umuhimu wa Urusi kuondoa vikosi vyao vyote na kuunga mkono juhudi za kumaliza mzozo kwa diplomasia,” Stoltenberg amewaambia waandishi wa habari.

“Tunatoa misaada kwa Ukreini na wakati huo huo NATO si sehemu ya mzozo. NATO ni umoja wa kujihami, hatutafuti mzozo wa kivita na Urusi.”

Blinken alisisitiza kuwa NATO na Marekani “hazitaki mgogoro.”

“Lakini kama mzozo ukija kwetu, tupo tayari,” aliongeza “na tutalinda hata inchi moja ya mipaka yetu.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

error: Content is protected !!