WANAWAKE wa ACT Tanzania waadhimisha siku ya wanawake Duniani kwa kuwatembelea wazazi katika Kituo cha Afya cha Palestina Sinza jijini Dar es salaam. Anaripoti Rhoda Kanuti, Dar es Salaam … (endelea).
Tukio hilo limefanyika leo Machi 4, 2022, ambapo sambamba na kuwatembelea pia waliwapelekea vitu mbalimbali kama vile sabuni, mafuta ya kupaka na nepi za watoto.
Akizungumza kwaniaba ya wenzake, Katibu Ngome ya Wanawake, Bonafasia Mapunda amesema wamekwenda kuadhimisha siku ya wanawake Duniani ambayo kaulimbiu ya mwaka huu inasema usawa wa kijinsia kwa maendeleo.
“Usawa wa kijinsia uko katika pande nyingi kama vile Uchumi, Kisiasa, na kijamii. Kwenye kijamii ndio tunaanzia kwenye kazi kubwa ya uumbaji hivyo tunahitaji kuwatia moyo wanawake kwasababu kama wameweza kuleta viumbe dunia basi wanaweza kufanya shughuli yoyote ya kijamii na kuleta maendeleo pia wanaweza kuingia kwenye siasa nakuwa viongozi bora,’’ amesema na kuongeza kuwa wameona waende kuwatembelea na kuwapa pongezi kwa kazi kubwa walioifanya yakuwaleta duniani watoto wakiume na wakike.
Mapunda alihitimisha kwa kumshukuru Meneja wa Wazazi kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kuwahudumia wanawake wanao leta watoto duniani.
Leave a comment