Friday , 10 May 2024
Home Kitengo Biashara Biteko: Mazingira uwekezaji sekta ya madini njia nyeupe
Biashara

Biteko: Mazingira uwekezaji sekta ya madini njia nyeupe

Spread the love

NAIBU Waziri Mkuu, Dk. Doto Biteko ametoa wito kwa wawekezaji kuja kuwekeza zaidi Tanzania katika shughuli za utafutaji, uchimbaji, uchenjuaji, uongezaji thamani na biashara ya madini. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Amesema Serikali itaendelea kushirikiana na wawekezaji wa ndani na nje kwa manufaa ya pande zote mbili.

Dk. Biteko ametoa kauli hiyo leo Jumatano kwa niaba ya Rais Samia Suluhu Hassan wakati akifungu kongamano la kimataifa la Madini na Uwekezaji Tanzania 2023 linalofanyika kwa siku mbili jijini  Dar es Salaam.

Amesema mazingira ya uwekezaji katika sekta ya madini yameendelea kuboreshwa na kuwa rafiki zaidi.

“Nafurahi kusema kuwa, hadi sasa jumla ya Kampuni tisa za Kimataifa za uchimbaji mkubwa wa madini zimeingia ubia na Serikali katika uchimbaji wa madini mbalimbali ikiwemo madini ya nikeli, kinywe, heavy mineral sands (mchanga bahari), Rare Earth Elements, dhahabu na almasi.).

Ameswma mkutano huo wenye kaulimbiu isemayo “Unlocking Tanzania’s Future Mining Potential” una lengo la kufungua hazina ya madini yaliyopo Tanzania kwa ajili ya uwekezaji kwa manufaa ya kiuchumi na kijamii.

“Kama mnavyofahamu kwa sasa ulimwengu unaendelea kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kwa kuhimiza matumizi ya teknolojia rafiki kwa mazingira. Teknolojia hizo kwa sehemu kubwa zinahitaji matumizi ya madini muhimu na ya kimkakati ambayo ni pamoja na madini ya nickel, copper, lithium,cobalt, graphite na rare earth elements (REE). Kwa bahati nzuri Tanzania imabarikiwa kuwa na madini hayo,” amesema.

Ameswma kutokana na taarifa ya Wakala wa Nishati wa Kimataifa (International Energy Agency) ya mwaka 2023, mahitaji ya madini ya kimkakati kwa ajili ya nishati safi yanatarajiwa kuongezeka mara tatu na nusu ifikapo 2030.

Hivyo, tunategemea shughuli za uvunaji wa madini hayo utaongezeka sehemu mbalimbali duniani ikiwemo Tanzania,” amesema.

Kwa upande wake, Waziri wa Madini, Anthony Mavunde amesema kuwa ili kuhakikisha nchi ya Tanzania inanufaika na rasilimali madini, Wizara  itaendelea kuimarisha usimamizi wa shughuli za Sekta ya Madini ili kuhakikisha inawanufaisha wananchi na Serikali inapata mapato stahiki.

“Wizara itaendelea kuimarisha

usimamizi wa shughuli za Sekta ya Madini ili kuhakikisha kuwa mchango wake unakua hadi kufikia asilimia 10 ya Pato la Taifa kufikia  mwaka 2025 kama ilivyo katika Dira ya Maendeleo ya Taifa ya Mwaka 2025. Tutashirikiana na wadau mbalimbali wa Sekta kuhakisha lengo hilo linafikiwa,” ameongeza Waziri Mavunde.

Kwa upande mwingine,  Mawaziri wa Madini kutoka nchini Malawi, Monica Chang’anamuno na Mhe.Peter Lokeres kutoka nchini Uganda wamesema kuwa Afrika ina fursa nyingi za Sekta ya Madini zinazovutia wawekezaji kuwekeza.

Mkutano wa Madini 2023 umehudhuriwa na mawaziri kutoka nje ya nchi, Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Nishati na Madini, Makatibu Wakuu na Manaibu Wakuu kutoa Tanzania Bara na Visiwani, Waheshimiwa Mabalozi, Viongozi wa Serikali, Vyama vya siasa na Wakuu wa Taasisi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Biashara

Meridianbet kasino yaja na promo ya mil 200/=

Spread the love  Kimbunga Hidaya kilikuja na madhara makubwa sana katika maeneo...

Biashara

Moon of Thoth, historia ya Misri ya kale ilipofichwa ndani ya kasino

Spread the love  Nchi ya Misri imebeba karibia asilimia kubwa ya mambo...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafugaji kuku Ihemi wanufaika na mafunzo

Spread the loveWADAU  wa mnyororo wa thamani katika sekta ndogo ya kuku...

Biashara

Expanse Tournament kasino mzigo umeongezwa hadi mil 400/=

Spread the love Jiunge na Meridianbet kasino kufurahia promosheni kubwaya Expanse Tournament,...

error: Content is protected !!