Monday , 11 December 2023
Home Habari Mchanganyiko Migodi 350 yaunganishwa na umeme wa gridi ya Taifa
Habari MchanganyikoTangulizi

Migodi 350 yaunganishwa na umeme wa gridi ya Taifa

Spread the love

Naibu Wazirj Mkuu, Dk. Doto Biteko amesema migodi zaidi ya 350 ya wachimbaji wadogo imeunganishwa na umeme wa gridi ya Taifa na hivyo kupunguza gharama za uzalishaji na kurahisisha shughuli mbalimbali za migodi. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Pia amesema hadi sasa baadhi ya migodi mikubwa ikiwemo Geita Gold Mines Limited (GGML) na STAMIGOLD Biharamulo Mine ambayo ilikuwa haina umeme kwa muda mrefu sasa imeunganishwa na umeme wa gridi ya Taifa.


Dk. Biteko ametoa kauli hiyo leo Jumatano wakati akifungua kongamano la kimataifa la madini na uwekezaji Tanzania 2023 linalofanyika kwa siku mbili tarehe 25,26 Oktoba mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Amesema Serikali inafahamu kuwa bado kuna mahitaji makubwa ya migodi kuunganishwa na umeme wa gridi ya Taifa hivyo inaendelea na kuboresha sekta hiyo.

“Napenda kuwahakikishia kuwa, kadri tunavyoimarisha uwezo wetu wa kuzalisha, kusafirisha na kusambaza umeme nchini, tutahakikisha migodi yote mikubwa na midogo inaunganishwa na umeme wa gridi ya Taifa.

“Pia Serikali inaendelea kuimarisha miundombinu ya usafirishaji ikiwa ni pamoja na ujenzi wa reli ya kisasa na barabara zinazounganisha maeneo yenye migodi na shughuli mbalimbali za madini ili kurahisisha usafirishaji wa bidhaa zinazoingia na kutoka migodini,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Amsons Group watoa milioni 100 waathirika maafa Hanang

Spread the loveKAMPUNI ya Amsons Group kupitia kampuni zake za Camel Oil...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Mpango: Sitakufa bali nitaishi

Spread the loveMAKAMU  wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk....

Habari Mchanganyiko

Kesi ya mfanyakazi wa CRDB itaendelea J’tatu

Spread the love  MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kinondoni, Dar es Salaam inatarajia...

Habari za SiasaTangulizi

Mbowe: Miaka 62 ya uhuru tujenge upya mioyo yetu

Spread the loveWAKATI Tanganyika ikiadhimisha miaka 62 tangu kupata uhuru, Mwenyekiti wa...

error: Content is protected !!