Monday , 27 May 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Binti achomwa moto hadi kufa
Kimataifa

Binti achomwa moto hadi kufa

Spread the love

NI binti wa miaka 18 ambaye alikimbia kwa zaidi ya mita 100 ili kujiokoa na shambulizi, hatimaye alianguka chini kwa uchovu, wauaji wakamfikia kisha wakamchoma moto mpaka mauti yakamfika. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia Februari 23, 2018 katika Kijiji cha Pradesh, Wilaya ya Unnao, India. Polisi wamethibitisha kutokea kwa tukio hilo. Binti huyo alitambulika kwa jina moja la Moni.

Moni alikuwa muuza mbogamboga, wakati wa tukio hilo, alikuwa barabarani akiendesha baiskeli yake akitoka sokoni kurejea nyumbani akiwa tayari kafunga biashara.

Ilikuwa usiku wa Alhamisi ya 22 Februari, 2018 ambapo Moni akiwa njiani, alikutana na watu ambao hawakutambulika haraka, walimfuata na kumzunguka huku wakiwa na kidumu cha petrol.

Walimsukuma kutoka kwenye baskeli yake na kuanguka chini kisha wakaanza kummimia petroli, alipata nguvu na kuanza kujitetea kwa kuwachoropoka watu hao na kukimbia.

Moni alikimbia kwa zaidi ya kilomita 100 usiku huo na taratibu alianza kuishiwa pumzi na hatimaye alianguka chini. Kuanguka kwake chini kulitoa nafasi kwa wauaji kuwasha njiti ya kibiriti na kumtupia, Moni aliwaka moto na kufa papo hapo bila kupata msaada kutoka kwa watu wengine.

Mkuu wa Polisi wa wilayani humo, Sujit Kumar Pandey alifika eneo la tukio usiku huo na baadaye kukutana na ndugu wa marehemu. Hata hivyo, polisi wamesema kuwa, bado wanafanya uchunguzi kama tukio hilo limetokana na uonevu ama uadui ndani ya familia.

Polisi wamekieleza Kituo cha Habari cha IANS kwamba, uchunguzi wa awali eneo la tukio umebaini kuwepo kwa kidumu cha petroli kilichotumika, kibiriti pamoja na matairi manne ya gari, tukio hilo lilitokea karibu na Tedha Bazaar nchini humo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifa

Ayatollah Khamenei aongoza wairan kumuaga Raisi

Spread the loveKiongozi wa Juu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei, ameongoza mjini...

AfyaKimataifaTangulizi

Waliowekewa damu yenye VVU, homa ya ini kulipwa fidia trilioni 32.9

Spread the loveWaziri mkuu wa Uingereza, Rishi Sunak ameahidi kulipa fidia ya...

Habari za SiasaKimataifa

Balozi Kasike ateta na mjumbe wa FRELIMO

Spread the loveBalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Msumbiji, Phaustine...

Kimataifa

Zuma akwaa kisiki, mahakama yamzuia kuwani urais

Spread the loveMahakama ya katiba nchini Afrika Kusini, katika uamuzi wake imesema...

error: Content is protected !!