MWANDISHI wa gazeti la Uhuru, Mariam Mziwanda amenusurika kifo katika ajali ya gari iliyotokea usiku huu maeneo ya Tabata jijini Dar es Salaam baada gari yake kugongwa na kubanwa na magari mawili. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).
Ajali hiyo imetokea majira ya saa 4:40 usiku huu maeneo ya TOT- Tabata baada ya gari lenye namba za usajiri T222 DJX alilokuwa akiendesha kufinywa na magari mawili na kukandamizwa na kontena.
Mariam baada ya ajali hiyo amekimbizwa katika hospitali ya Muhimbili kwa ajili ya matibabu na Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea aliyefika eneo la ajali muda mfupi baada ya kutokea ajali hiyo.
Kwa mujibu wa Kubenea, alimkuta Mariam akiwa tayari ametoka katika ajali hiyo, akilalamika maumivu makali kifuani, hivyo kulazimika kumkimbiza hospitali kwa matibabu zaidi.
Leave a comment