Tuesday , 7 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Bilioni 50 kupanua kiwanja cha ndege Kigoma
Habari Mchanganyiko

Bilioni 50 kupanua kiwanja cha ndege Kigoma

Spread the love

JUMLA ya Sh bilioni 50 zinatarajiwa kutumika katika upanuzi wa Kiwanja cha Ndege Kigoma kwa kurefusha barabara ya kuruka na kutua ndege kutoka ya sasa yenye mita 1800 hadi kufikia mita 3000 na kuruhusu kiwanja hicho kuhudumia ndege kubwa zaidi zenye uwezo wa kubeba abiria zaidi ya 150.

Fedha hizo pia zitahusisha upanuzi wa barabara ya kuruka na kutua ndege, maegesho, uzio na malipo ya fidia. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Akizungumza mkoani Kigoma mara baada ya kutembelea Kiwanja hicho Naibu Waziri wa Uchukuzi, Atupele Mwakibete amesema Serikali imedhamiria kufufua usafiri wa anga nchini kwa kununua ndege na kuboresha viwanja vya ndege ili kurahisisha shughuli za biashara na utalii baina na mikoa na nchi jirani.

Naibu Waziri wa Uchukuzi, Atupele Mwakibete akimsikiliza Kaimu Meneja wa Kiwanja cha Ndege cha Kigoma, Mbura Daniel kuhusu utendaji wa Kiwanja hicho wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea Kiwanja cha Ndege hicho Mkoani Kigoma.

“Serikali inaendelea na mkakati wake wa kuendelea kujenga viwanja vya ndege nchini hasa ukizingatia Rais alifanya filamu ambayo matokeo yake yameanza kuonekana na hatuna budi kuendelea kujenga miundombinu rafiki na mizuri kwenye kila eneo’ amesema Naibu Waziri Mwakibete.

Naibu Waziri Mwakibete amewapongeza Mamlaka ya Viwanja vya Ndege kwa kuendelea kufanya maboresho katika viwanja mbalimbali nchini na kuwataka kuendelea kushirikiana na vyombo vingine ili kuhakikisha wanadhibiti usafirishaji wa nyara za Serikali.

Kwa upande wake Mbunge wa Kigoma Mjini, Kilumbe  N’genda (CCM) ameishukuru Serikali na kusema Kigoma itaendelea kufunguka kibiashara na kukuza pato kwani nchi Jirani kama Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo na Burundi zinafanya sana biashara na mkoa wa Kigoma.

Kaimu Meneja wa Kiwanja cha Ndege cha Kigoma, Mbura Daniel amesema idadi ya miruko ya ndege imekuwa ikiongezeka kwani hicho pamoja na kutumiwa na ndege za ratiba kama Air Tanzania pia mashirika mbalimbali hukitumia kiwanja hicho kwa kuja kufanya biashara na mikutano ya Kimataifa.

Meneja wa Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL), Mkoa wa Kigoma Mwantum Kipwasa amesema shirika linasubiri kwa hamu kukamilika kwa upanuzi huo ili kuleta ndege kubwa kwani idadi ya abiria imelazimisha shirika hilo kuwa na ndege kila siku ili kukidhi haja ya wateja wao.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Samia aagiza huduma za dharura maeneo yaliyoathiriwa na kimbunga Hidaya

Spread the love   RAIS wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Samia...

Habari Mchanganyiko

Mahakama yatoa uamuzi zuio dhidi ya Club House

Spread the loveMAHAKAMA Kuu ya Tanzania, Masjala Kuu jijini Dar es Salaam,...

Habari Mchanganyiko

GGML, OSHA yawanoa bodaboda 200 Arusha

Spread the loveZAIDI ya madereva bodaboda 200 wa jiji la Arusha wamepatiwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Serikali kuwakopesha wajasiriamali 18.5bn/- kupitia NMB

Spread the loveSerikali imetenga kiasi cha Sh 18.5 bilioni kwa ajili ya...

error: Content is protected !!