Friday , 3 May 2024
Home Kitengo Maisha Afya Bilioni 5.9 zatumika kununua viuadudu
Afya

Bilioni 5.9 zatumika kununua viuadudu

Spread the love

SERIKALI kupitia Wizara ya Afya imetumia kiasi cha Sh 5.9 bilioni kununua viuadudu katika ngazi ya Halmashauri ndani ya kipindi cha mwaka 2017 hadi 2023. Anaripoti Mlelwa Kiwale,TUDARCo…(endelea).

Hayo yaimebainishwa leo Ijumaa Bungeni Jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Afya, Dk. Godwin Mollel wakati akijibu maswali ya Wabunge katika kikao cha Bunge la 12.

Dk. Mollel amesema ili kuhakikisha uhakika wa upatikanaji wa viuadudu kutoka kiwanda cha Kibaha kwa kipindi cha mwaka 2024-2026, Wizara ya Afya imeomba kupatiwa jumla ya Sh  129.1 bilioni kwa ajili ya utekelezaji wa afua ya unyunyiziaji wa viuadudu ili kuangamiza viluilui wa mbu kwenye mazalia ili kufikia lengo la kutokomeza malaria ifikapo 2030.

“Wizara ya Afya inashirikiana na Shirika la Taifa la Maendeleo ya Viwanda kuhakikisha Kiwanda kinapata ithibati kutoka Shirika la Afya Duniani ili kuongeza wigo wa upatikanaji wa fedha za kutekeleza wa afua hii kutoka kwa wadau mbalimbali wa mapambano dhidi ya ugonjwa wa Malaria,” ameeleza Dk. Mollel.

Aidha, Dk. Mollel amesema Serikali imeendelea kuboresha upatikanaji wa dawa na vifaa tiba katika hospitali zote ili kutatua changamoto ya dawa nchini.

Katika kutatua changamoto ya dawa nchini Dk. Mollel amesema serikali imeanza utekelezaji wa kuipatia mtaji Bohari ya Dawa kwa mwaka wa fedha 2023/2024 ili kuwa na bidhaa za Afya muda wote.

Ameongeza kuwa Serikali imetoa fedha za ununuzi wa bidhaa za afya kila mwezi kwa ajili ya vituo vya kutolea huduma za Afya vya Umma ili kukabiliana na upungufu wa dawa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

AfyaHabari Mchanganyiko

Songwe katika mikakati ya elimu ya lishe kudhibiti udumavu

Spread the love  SERIKALI mkoani Songwe imejipanga kuendelea kutoa elimu ya lishe...

Afya

Mloganzila yajipanga kupandikizaji wa ini

Spread the love  HOSPITALI ya Taifa Muhimbili-Mloganzila imesema kutokana na uwekezaji uliofanywa...

AfyaHabari za Siasa

Serikali yasaka watumishi afya ngazi ya jamii 8,900

Spread the loveSERIKALI imeanza utekelezaji wa mpango jumuishi wa wahudumu wa afya...

error: Content is protected !!