Saturday , 30 September 2023
Home Habari Mchanganyiko Nyongeza ya pensheni kiwango cha chini 100,000
Habari Mchanganyiko

Nyongeza ya pensheni kiwango cha chini 100,000

Patrobas Katambi
Spread the love

SERIKALI imesema wastaafu wote wameboreshewa pensheni zao za kila mwezi, ambapo kiwango cha chini kwa sasa ni Sh 100,000. Anaripoti Maryam Mudhihiri…(endelea)

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Uemavu), Patrobas Katambi alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Nancy Nyalusi aliyetaka kujua ni lini serikali itaboresha mafao ya wastaafu kwa kuongeza kipato cha pensheni anayopata mstaafu kila mwezi.

“Mifuko ya Hifadhi ya Jamii huongeza kiwango cha pensheni ya kila mwezi kwa wastaafu mara baada ya kufanya tathmini na kujua uendelevu wake na uwezo wa kulipa mafao kwa wanachama wake.

“Tathmini hiyo hufanyika kila baada ya miaka mitatu kwa kipindi kifupi, miaka mitano kwa kipindi cha kati na tathmini ya kipindi kirefu ni miaka kumi.

“Mheshimiwa Spika, Kanuni za ulipaji mafao Namba 11(1) za mwaka 2018 zilielekeza Mifuko ya Hifadhi ya Jamii kuongeza pensheni kwa kuzingatia mfumuko wa bei na uendelevu wa Mfuko kila baada ya miaka mitatu.

“ Hata hivyo, ninayo furaha kuliarifu Bunge lako kuwa hadi sasa wastaafu wote wa Serikali walishaboreshewa pensheni zao za kila mwezi, ambapo kiwango cha chini ni Sh 100,000 na kuendelea tofauti na hapo awali,” amesema Naibu Waziri huyo.

1 Comment

  • Wameongeza lini mbona hatujaona hiyo nyongeza? Ebu nyie MwanaHalisi tuulizeni wastahafu wa serikali. Ni uongo mtupu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Askari Polisi wa wanawake watakiwa kuchangamkia fursa za elimu

Spread the love  KAMISHNA wa Polisi Utawala Menejimenti ya rasilimali watu, CP...

Habari Mchanganyiko

Vijana 400 waguswa na programu ya “Learning for Life” ya SBL

Spread the love  PROGRAMU ya “Learning for Life” imetimiza dhamira ya Serengeti...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Stamico yafungua fursa za kiuchumi kwa makundi maalumu

Spread the loveSHIRIKA la Madini la Taifa (STAMICO) limemwaga neema kwa watu...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Maabara ya bilioni 5 upimaji madini yazinduliwa Geita, inapima kwa mionzi

Spread the loveZaidi ya Sh bilioni tano zimewekezwa katika kampuni ya MSALABS...

error: Content is protected !!