Monday , 11 December 2023
Home Kitengo Maisha Elimu Bihimba asaidi ujenzi shule, wadau wengine waitwa
Elimu

Bihimba asaidi ujenzi shule, wadau wengine waitwa

Spread the love

MWANAHARAKATI huru, Bihimba Nasoro Mpaya, imesaidia ujenzi wa ukuta wa shule ya Sekondari ya Abbuy Jumaa, iliyoko Kivule jijini Dar es Salaam, kwa kuipatia matofali 500 yenye thamani ya Sh. 500,000, pamoja na mifuko ya saruji 20. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Bihimba amekabidhi vifaa hivyo vya ujenzi leo tarehe 19 Oktoba 2023, katika mahafali ya 14 ya wanafunzi wa kidato cha nne, yaliyofanyika shuleni hapo baada ya Mkuu wake wa shule, Froida Nkya, kuwaomba wadau watoe misaada itakayosaidia kutatua changamoto zinazoikabili.

Mwanaharakati huyo amesema kuwa,ameamua kutoa mchango huo ili kusaidia kuboresha mazingira mazuri ya shule, yatakayowasaidia watoto kusoma vizuri pamoja na walimu wake kufanya kazi kwa moyo.

“Hii si mara ya kwanza kuisaidia shule hii, hadi sasa nimeshatoa mifuko 20 ya saruji pamoja na matofali 500, kwa ajili ya ujenzi wa ukuta ambao umekwama, naamini ukuta huu ukimalizika changamoto za watoto kutoroka na hata ukosefu wa ulinzi na usalama shuleni itapungua,” amesema Bihimba na kuongeza:

“Hii shule ni ya wananchi, wenye mamlaka ni wananchi ambao ni wazazi wenye watoto wanaosoma pale hivyo inapaswa kujengwa kwa nguvu zao. Kweli serikali ipo lakini wananchi tunapaswa kusaidia vitu vidogovidogo.”

Mbali na Bihimba, wananchi mbalimbali walifanya harambee kwa ajili ya kuchangisha fedha za ujenzi wa ukuta, ambapo zilipatikana zaidi ya Sh. 400,000, huku wengine wakiahidi kutoa matofali na vifaa vingine.

Mgeni rasmi katika mahafali hayo, Dk. Katanta Simwanza, aliahidi kutoa kompyuta tatu, kuunganisha hsule hiyo na huduma ya intanenti, pamoja na kuwatafuta wadau wengine zaidi kwa ajili ya kuisaidia shule hiyo.

Awali, Nkya aliwaomba wadau watoe michango yao ya hali na mali kwa ajili ya kutatua changamoto hizo, ikiwemo uhaba wa matundu ya vyoo 50 ambapo kwa sasa viko 14 na vinavyohitajika ni 64. Chumba cha wanafunzi na walimu wa kike kujihifadhi wakiwa katika siku za hedhi na vifaa vya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), hususan kompyuta.

“Tunamshukuru Bihimba kwa kutoa msaada huu ambao utatusogeza kidogo kwenye ujenzi wa ukuta, lakini bado tunahitaji misaada mingine,” amesema Nkya.

Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya Sekondari ya Abuuy Jumaa, Emanuel  Kimaro, amesema shule hiyo inakwamba kutatua changamoto ndogondogo kutokana na wazazi na walezi wa wanafunzi kuwa wazito kutoa michango itakayowezesha kuitatua.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

ElimuTangulizi

Mwalimu Maganga Japhet asimamishwa kazi kwa utoro

Spread the loveMwalimu Maganga Japhet amesimamishwa kazi na Tume ya Utumishi wa...

ElimuHabari Mchanganyiko

CEO NMB awataka vijana kunoa ujuzi wao

Spread the loveAfisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna, amewashauri...

Elimu

150 wahitimu Shahada ya Udaktari HKMU

Spread the loveCHUO Kikuu cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki (HKMU), kimeiomba serikali...

Elimu

Aliyehitimu udaktari HKMU na miaka 21 atoa siri

Spread the love MHITIMU wa fani ya udaktari ambaye ni mdogo kuwahi...

error: Content is protected !!