Sunday , 28 April 2024
Home Habari Mchanganyiko RC Dar: Chanzo ajali ya moto Kariakoo ni hujuma
Habari MchanganyikoTangulizi

RC Dar: Chanzo ajali ya moto Kariakoo ni hujuma

Spread the love

CHANZO cha ajali ya moto ulioteketekeza Soko la Kariako eneo la Mnadani na kusababisha hasara kubwa kwa wafanyabiashara zaidi ya 550, kimetajwa kuwa ni hujuma za baadhi ya wafanyabiashara. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Hayo yamebainishwa leo tarehe 20 Oktoba 2023 na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila akitaja matokeo ya uchunguzi uliofanywa na kamati aliyounda kuchunguza chanzo cha tukio hilo lililotokea tarehe 1 Oktoba mwaka huu.

“Kamati imebaini kwamba moto huo haikuwa ajali bali ilikuwa ni hujuma ndani ya wafanyabiashara wenyewe na moto ulianzia katika eneo la mnadani. Maelezo haya yote yamebainika katika baadhi ya kamera za CCTV ambazo zilikuwa pembezeno wakati moto unaanza taratibu kabla haujaingia maeneo mengine,” amesema Chalamila.

Chalamila amesema “awali wafanyabiashara walisema umesababishwa na jenereta ambalo lilikuwepo pembezoni mwa maeneo hayo, lakini uchunguzi umebaini ni zima na linafanya kazi. Halikuungua wala hakikuwa chanzo cha moto huo.”

Hata hivyo, Chalamila hakuweka bayana namna hujuma hizo zilivyofanyika na kusababisha tukio hilo.

Chalamila ameagiza uchunguzi ufanyike ili kubaini watu wanaodaiwa kuchoma moto soko la Kariakoo.

“Navielekeza vyombo vyote sasa vinavyoshughulika na masuala yanayohusiana na uvunjifu wa sheria viweze kuanza kazi yake mara moja kubaini watu waliofanya hivyo na kusababisha hasara.”

Akielezea namna kamati hiyo ilivyofanya uchunguzi wake, Chalamila amesema walichunguza eneo la tukio pamoja na kufanya mahojiano na baadhi ya mashuhuda, wafanyabiashara, wamiliki na walinzi wlaiokuwa zamu wakati tukio linatokea.

Mkuu huyo wa Dar es Salaam amesema kamati imetoa mapendekezo kadhaa kufuatia tukio hilo, ikiwemo halmashauri ya jiji hilo kuzingatia sheria ya upangaji majengo kwa kuweka njia za dharura ili kuweza kushughulikia matukio kama hayo kirahisi.

Pia imeshauri wafanyabiashara waliokuwa katika eneo hilo watafutiwe eneo lingine, pamoja na uchunguzi ufanyike kujua wamiliki halali wa biashara zilizoathirika.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mvungi aendesha kikao kazi cha wataalam wa Regrow

Spread the love  MKURUGENZI wa Idara Sera na Mipango Wizara ya Maliasili...

Habari MchanganyikoTangulizi

Jacob, Malisa waachiwa kwa masharti

Spread the love  JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

Habari Mchanganyiko

Polisi wakanusha kufanya uzembe ajali iliyouwa mwandishi Ayo Tv

Spread the loveJESHI la Polisi limekanusha tuhuma zilizoibuliwa dhidi yake  kwamba limekawia...

error: Content is protected !!