Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Ongezeko la wanawake magerezani lashtua, watetezi haki binadamu waja juu
Habari Mchanganyiko

Ongezeko la wanawake magerezani lashtua, watetezi haki binadamu waja juu

Spread the love

Washiriki katika Kongamano la Mashariki mwa Afrika kuhusiana na haki za wanawake katika masuala ya jinai lililofanyika nchini Uganda, wameelezea wasiwasi wao kuhusu kasi ya ongezeko la wanawake wafungwa magerezani. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa …(endelea)

Ili kukabiliana na hali hiyo kwa kuzingatia jinsia na majukumu ya wanawake katika jamii, wadau kutoka mataifa hayo wanakutana mjini Kampala kubuni na kuwasilisha mapendekezo kwa nchi za Afrika kuchunguza upya jinsi kesi na hukumu kwa wanawake zinavyotakiwa kuzingatia maslahi yao.

Mmoja wa waathirika wa hukumu za kesi za jina ni Roselyn Kodet ambaye amedai Mahakama haikuzingatia chanzo cha yeye kutenda mauaji bila kukusudia.

Alihukumiwa miaka saba akiwaacha ndugu zake aliokuwa akiwatunza ambao pia ni yatima pamoja na wanawe baada ya mumewe kuugua ugonjwa wa akili.

Ni katika hali hii ndipo Grace Dafa kutoka Kituo cha Msaada wa Sheria kutoka Tanzania anasema ni “muhimu kuwachukulia wanawake wafungwa na pia wale wanaokutwa wamevunja sheria kuwa kundi ambalo linahitaji kuchunguzwa kilichowasababisha kushiriki vitendo vya jinai.”

Kwa mujibu wa Kamishna Mkuu wa Magereza ya Uganda, Johnson Byabashaija theluthi moja ya kesi za wanawake wafungwa katika magereza ya Uganda ni zinahusiana na mauaji.

“Jamii ichunguze na kushughulikia vyanzo vya hali hiyo. Sisi kama magereza huzuia kuwashughulikia wanawake wafungwa kwa sababu wana mahitaji maalum kutokana na jinsia yao pamoja na majukumu ya kuwalea watoto,” amesema mkuu huyo wa magereza.

Wadau kutoka mataifa mbalimbali ikiwemo Rwanda na Kenya walikuwa wanakutana kubadilishana uzoefu na mikakati ya kuwasaidia wanawake wanaokabiliwa na mashtaka ya jinai kurejelea maisha ya kawaida.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

RPC Dodoma akabidhiwa bunduki mbili za wahalifu

Spread the love  Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa ya Kulevya...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yazindua huduma maalum kwa wastaafu

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imezindua huduma maalum kwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yazindua akaunti ya Kikundi

Spread the loveBenki ya NMB imezindua akaunti ya kikundi yenye  maboresho makubwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyakazi waidai STAMICO mishahara ya bilioni 1

Spread the loveWALIOKUWA wafanyakazi wa mgodi wa Shirika la Madini la Taifa...

error: Content is protected !!