Monday , 11 December 2023
Home Kitengo Habari Kimataifa Viongozi wa Hamas wauawa, vifo vyafikia 3,785.
KimataifaTangulizi

Viongozi wa Hamas wauawa, vifo vyafikia 3,785.

Spread the love

TANGU vita baina ya taifa la Israel na wanamgambo wa Hamas kutoka Ukanda wa Gaza nchini Palestina viibuke tarehe 7 Okotoba 2023, kumeripotiwa mkururo wa vifo vya viongozi wa kundi hilo linalotajwa kuwa la kigaidi.

Vyombo vya habari vinavyohusiana na Hamas vimesema kuwa mkuu wa vikosi vya usalama vya Hamas ameuawa huko Gaza.

Watu wa familia ya Jehad Mheisen pia wanaripotiwa kufariki. Mjane wa mwanzilishi mwenza wa Hamas, Abdel Aziz al-Rantisi pia anaripotiwa kuuawa usiku wa kuamkia jana.

Aidha, Jeshi la Israel limesema ndege zake za kivita zilishambulia maeneo zaidi ya 100 na kumuua mwanachama mmoja wa Hamas ambaye inaaminika huenda alishiriki katika uvamizi huo wa tarehe 7 Oktoba  uliosababisha vifo vya watu 1,400 nchini Israel.

Hizo takwimu za hivi punde zaidi za wanachama wa Hamas waliofariki katika kile Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu amekitaja kuwa ni vita vya muda mrefu ambavyo nchi yake inaendesha dhidi ya Hamas.

Siku ya Jumatano, shirika la habari la AFP liliripoti kuwa Jamila Al-Shantee, mwanamke wa kwanza kuchaguliwa katika uongozi wa kisiasa wa Hamas aliuawa katika shambulio la Israel.

Mapema wiki hii, Vikosi vya Ulinzi vya Israel vilisema katika chapisho kwenye X, zamani Twitter, kwamba Ayman Nofal, aliyetajwa kama “afisa mkuu wa Hamas”, pia aliuawa.

Hayo yanajiri wakati Israel ikiendeleza mashambulizi dhidi ya kundi la Hamas katika Ukanda wa Gaza na hadi sasa idadi ya vifo inadaiwa kufikia watu 3,785.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Mpango: Sitakufa bali nitaishi

Spread the loveMAKAMU  wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk....

Habari za SiasaTangulizi

Mbowe: Miaka 62 ya uhuru tujenge upya mioyo yetu

Spread the loveWAKATI Tanganyika ikiadhimisha miaka 62 tangu kupata uhuru, Mwenyekiti wa...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia ataka jamii inayohoji mafisadi

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan ametoa maagizo juu ya uboreshaji dira...

Habari za SiasaTangulizi

Kapinga: Kukatika kwa umeme siyo hujuma

Spread the loveNaibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga amesema Serikali ipo kazini...

error: Content is protected !!