Tuesday , 7 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Benjamini Mkapa yaokoa bilioni 3.881 matibabu ya kibingwa
Habari Mchanganyiko

Benjamini Mkapa yaokoa bilioni 3.881 matibabu ya kibingwa

Spread the love

HOSPITALI ya Benjamini Mkapa iliyopo Jijini Dodoma imeokoa kiasi cha Sh. bilioni 3.881 tangu ilipoanza kutoa huduma ya upandikizaji wa figo, upanuaji wa nyonga na magoti pamoja na uvunja wa mawe kwenye figo. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma… (endelea).

Hayo yameelezwa na jana tarehe 26 Oktoba, 2022 na Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamini Mkapa Dk. Alphonce Chandika alipozungumza na waandishi wa habari Jijini Dodoma kuhusu utekelezaji wa mpango wa maendeleo kwa mwaka wa fedha 2021/22.

Amesema kutokana na serikali kuiwezesha upatikanaji wa vifaa vya kisasa katika hospitali hiyo, kwa sasa imetoa matibabu ya upandikizaji wa figo.

Amesema katika utoaji wa huduma kibingwa jumla ya wanufaika 31 wamepata huduma ya kupandikizwa figo bila kwenda nje ya nchi kama ilivyokuwa hapo awali.

Amesema iwapo mgonjwa mmoja angesafirishwa kwenda nchini India kwa kupandikizwa figo angelipia Sh milioni 100 wakati wao wanatoa huduma hiyo kwa gharama ya sh milioni 25 hivyo kwa watu 31 wameokoa zaidi ya  Sh.bilioni 1.3.

Aidha, amesema wagonjwa 715 wamefanyiwa uchunguzi wa magonjwa ya moyo bila kufunguliwa kifua na kati ya hao 39 wamebainika kuwa na matatizo ya kuziba mishipa ya moyo ya kupitisha damu na wagonjwa wawili walihudumiwa kwa dharura.

Sambamba na hilo Dk Chandika ameeleza kuwa Hospitali ya Benjamini Mkapa imewapandikiza betri ya kusukuma mapigo ya moyo wagonjwa nane ambao wanaendelea vyema na kuepukana kutafuta matibabu nje ya nchi.

Akizungumzia matibabu ya nyonga na magoti Dk. Chandika amesema wagonjwa 56 wamepatiwa matibabu ambapo wametibiwa kwa gharama ya Sh. milioni 12 kila mmoja na kama mgonjwa angeenda kutibiwa nchini India angetumia Sh. milioni 35 hivyo kwa kutoa matibabu hayo wameokoa kiasi cha Sh. bilioni 1.28.

Kuhusu upasuaji wa mawe kwenye figo kwa kutumia mionzi na miale amesema wagonjwa 148 wamehudumiwa bila kwenda India ambapo kama mgonjwa mmoja angetibiwa nchini humo angetumia Sh milioni saba wakati wao wanatibu kwa Sh. milioni 1.7 na kuokoa Sh. milioni 850 kwa wagonjwa wote waliotibiwa nchini.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari MchanganyikoMakala & Uchambuzi

Kisukari cha mimba ni nini?

Spread the loveKisukari cha mimba ni aina ya kisukari kinachotokea kwa baadhi...

Habari Mchanganyiko

Mafunzo kwa bodaboda 395 yamkuna Meya Dodoma

Spread the loveNAIBU Meya wa Jiji la Dodoma, Asma Karama amepongeza mafunzo...

Habari Mchanganyiko

Samia aagiza huduma za dharura maeneo yaliyoathiriwa na kimbunga Hidaya

Spread the love   RAIS wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Samia...

Habari Mchanganyiko

Mahakama yatoa uamuzi zuio dhidi ya Club House

Spread the loveMAHAKAMA Kuu ya Tanzania, Masjala Kuu jijini Dar es Salaam,...

error: Content is protected !!