Thursday , 2 May 2024
Home Kitengo Biashara Bei ya mafuta yapaa kwa mwezi Aprili
BiasharaTangulizi

Bei ya mafuta yapaa kwa mwezi Aprili

Spread the love

BEI za mafuta zimeongezeka kwa mwezi Aprili 2024, ikilinganishwa na bei elekezi zilizotangazwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), kwa mwezi uliopita. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Kwa mujibu wa bei elekezi zilizopangwa kutumika kuanzia tarehe 3 Aprili 2024, mafuta ya petroli imeongezeka kwa wastani wa Sh. 94, wakati ya dizeli ikipanda kwa wastani wa Sh. 84, huku mafuta ya taa yakibaki katika bei ya awali.

Mkoa wa Dar es Salaam, bei ya petroli imepanda kutoka Sh. 3,163 iliyotumika Machi, hadi kufikia Sh. 3,257 itakayotumika Aprili. Dizeli imepanda kutoka Sh. 3,126 (Machi) hadi kufikia Sh. 3,210.

Upande wa Mkoa wa Tanga, bei ya Petroli imeongezeka hadi kufikia Sh. 3,303 kutoka Sh. 3,209 iliyotumika Machi mwaka huu.

Taarifa iliyotolewa leo tarehe 3 Aprili 2024 na Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Dk. James Mwainyekule, imesema ongezeko la bei limetokana na kuongezeka kwa bei ya mafuta katika soko la dunia kwa wastani wa asilimia 3.94 kwa mafuta ya petroli na wastani wa asilimia 2.34 kwa dizeli.

“Mabadiliko ya bei yamechangiwa na kuongezeka kwa bei za mafuta yaliyosafishwa katika soko la dunia kwa wastani wa 3.94% kwa mafuta ya petroli na wastani wa 2.34% kwa mafuta ya dizeli, kupungua kwa gharama za kuagiza mafuta kwa wastani wa 4.28% kwa mafuta ya petroli na kuongezeka kwa wastani wa 0.76% kwa mafuta ya dizeli kwa bandari ya Dar es Salaam,” imesema taarifa hiyo.

Sababu nyingine ni “kuongezeka kwa wastani wa 13.73% kwa mafuta ya petroli na dizeli kwa Bandari ya Tanga na kuongezeka kwa wastani wa 12.71% kwa mafuta ya petroli na dizeli kwa Bandari ya Mtwara.

“Aidha, mabadiliko hayo yamechangiwa na kuongezeka kwa kiwango cha kubadilishia fedha za kigeni kwa asilimia 3.19 kutokana na ongezeko la matumizi ya sarafu ya Euro kulipia mafuta yaliyoagizwa,” imesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yashiriki maadhimisho Mei Mosi Arusha

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeungana na maelfu ya...

Biashara

Promosheni ya bil 1 kutoka Meridianbet kasino, cheza na ushinde zawadi kubwa

Spread the love  INGIA katika ulimwengu wa zawadi za kushangaza: Jishindie sehemu...

error: Content is protected !!