Friday , 3 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mahakama ya katiba Uganda kuamua hatima ya mashoga
Habari za SiasaKimataifa

Mahakama ya katiba Uganda kuamua hatima ya mashoga

Spread the love

Mahakama ya katiba ya Uganda leo Jumatano inatarajiwa kutoa uamuzi juu ya ombi la kutaka kubatilisha Sheria kali ya Kupambana na Ushoga nchini humo (AHA). Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Uamuzi huo unaweza ukachangia kuongezeka kwa adhabu kali dhidi ya mashoga kote barani Afrika, ikiwa ni pamoja na nchini Ghana ambapo wabunge pia walipitisha sheria dhidi ya mashoga mwezi Februari.

Kupitishwa kwa sheria ya kupinga mapenzi ya watu wa jinsia moja nchini Uganda mwezi Mei mwaka jana, kulizua vikwazo mbalimbali kutoka kwa jumuiya ya kimataifa, vikiwemo kutoka Benki ya Dunia na Marekani.

Benki ya Dunia ilisitisha utoaji wa mikopo mipya kwa nchi hiyo huku Marekani ikitangaza tahadhari za usafiri.

Chini ya sheria ya AHA vitendo vya jinsia moja na shughuli zinazohusiana navyo, huvutia adhabu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kifo kwa kosa la ulawiti uliokithiri, huku mapenzi ya jinsia moja adhabu yake yaweza kuwa kifungo cha maisha.

Kwa mujibu wa mmoja wa mawakili watetezi wa haki za mashoga nchini humo, Nicholas Opiyo amesema uamuzi huo unatarajiwa kutolewa leo mchana.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza uchaguzi mdogo Jimbo la Kwahani

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi, imetangaza uchaguzi mdogo...

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

error: Content is protected !!