Thursday , 2 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Askofu Malasusa asimikwa rasmi mkuu KKKT, aweka msimamo ukaribu wake na Serikali
Habari za SiasaTangulizi

Askofu Malasusa asimikwa rasmi mkuu KKKT, aweka msimamo ukaribu wake na Serikali

Spread the love

HATIMAYE  Mkuu wa Kanisa la Kiinjili  na Kilutheri Tanzani (KKKT) Askofu Dk. Alex Malasusa amesimikwa rasmi leo Jumapili na kubainisha msimamo wake kwamba hawezi kukataa ukaribu wake na Serikali kwa sababu hakulelewa kwenda kinyume au kutoitii Serikali. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Askofu Malasusa aliyechaguliwa na Mkutano mkuu wa 21 wa KKKT tarehe 25 Agosti mwaka jana kuchukua nafasi ya Askofu Dk. Fredrick Shoo aliyemaliza muda wake, amesimikwa katika Ibada Maalumu iliyofanyika katika Viwanja vya Kanisa Kuu la Azania Front, Dayosisi ya Mashariki na Pwani.

Akizungumza katima ibada hiyo iliyohudhuriwa na waumini na wageni  mbalimbali akiwamo Rais Samia Suluhu Hassan, Askofu Malasusa amesema ushiriki wa mkuu huyo wa nchi katika ibada hiyo kunaonesha namna gani dini na serikali vinaweza kushirikiana katika mambo mbalimbali kwa amani na upendo.

Amesema alipochaguliwa muumini mmoja alimtumia salamu za pongezi na kusema ” mitaani watu wanasema wewe uko karibu sana na Serikali”

Askofu Malasusa amesema hawezi kukataa ukaribu wake na Serikali kwa Sababu hukulelewa kwenda kinyume au kutoitii Serikali

Aidha, akihubiri katika lbada hiyo Maalumu, Askofu Dk. Samraj wa Kanisa la Kinjili la Kilutheri la Tamil, nchini India, amesisitiza maombi, umoja kwa wakristo wote bila kujali tamaduni, rangi ya ngozi au jografia.

Askofu huyo amempongeza Mkuu Mpya wa KKKT, Dk. Malasusa, ambaye amemtaja kuwa kama ndugu yake sasa kupitia kuunganishwa na Kristo.

Amemtaka Dk.Malasusa kusema ukweli na kutoogopa katika kuitenda kazi ya Mungu, kwa sababu si yeye aliyejichagua bali na Mungu mwenyewe kama alivyoeleza katika Waraka wa Yohana 15:16.

“Dk, Malasusa, umechaguliwa na Mungu, enenda ukazae matunda. Usiogope, kwa sababu neema ya Mungu yatosha, tumtumaini yeye,” amesema Askofu Samraj.

Akiongoza jukumu la kumsimika Dk Malasusa, Askofu Fredrick Shoo anayemaliza muda wake, amesema ameliacha kanisa mikononi mwake na anakwenda kutumikia dayosisi yake kwa ukaribu.

“Nimemaliza muda wangu, sasa ni muda wangu wa kuitumikia Dayosisi ya Kaskazini kwa ukaribu zaidi. Tulipokuchagua pale Makumira, wewe Dk. Malasusa kuwa mkuu mpya wa kanisa utakuwa na jukumu la kutekeleza wajibu kama inavyoonekana katika kanuni ya 12 ya kifungu A ya katiba ya kanisa hili,” amesema Askofu Shoo.

Mbali na Rais Samia, viongozi wengine wakuu wa Serikali waliohudhuria ibada hiyo ni pamoja na Spika Dk. Tulia Ackson, Jaji Mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Juma, Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi, Waziri wa mambo ya Ndani, Hamad Masauni na Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza uchaguzi mdogo Jimbo la Kwahani

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi, imetangaza uchaguzi mdogo...

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

error: Content is protected !!