Friday , 3 February 2023
Home Kitengo Habari Kimataifa Askari mbaroni kwa kumrekodi video mwanamke akiwa msalani
Kimataifa

Askari mbaroni kwa kumrekodi video mwanamke akiwa msalani

Mark Mutongoi
Spread the love

 

ASKARI mmoja wa kampuni binafsi ya ulinzi nchini Kenya, ameburuzwa katika mahakama ya Kibera kwa tuhuma za kumrekodi mwanamke akiwa msalani katika mtaa wa Westlands jijini Nairobi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Nairobi … (endelea)

Askari huyo Mark Mutongoi ambaye ni mlinzi katika kituo cha mafuta cha Rubis kilichoko katika mitaa hiyo ya Westlands, alipandishwa kizimbani jana tarehe 18 Oktoba, 2021 kwa tuhuma za kumrekodi video Margret Wangari bila ridhaa yake.

Askari huyo alimweleza Hakimu Charles Mwaniki kuwa wakati anatenda kosa hilo alikuwa ameingiwa na pepo mbaya.

Akisoma karatasi ya maelezo ya shtaka hilo, Mwendesha mashtaka wa mahakama hiyo, Robert Ogallo amesema askari huyo alimrekodi video Margret Wangari kwa makusudi bila idhini yake.

Alisema alifanya kosa hilo tarehe 7 Oktoba, 2021 katika kituo cha mafuta cha Rubis kilicho katika mtaa wa Westlands.

Akijitetea mbele ya mahakama hiyo, Askari huyo alidai kuwa alimrekodi mwanamke huyo ili kufurahisha macho yake.

Akifafanua kwa kina, Mwendesha mashtaka huyo amesema mlalamikaji yaani Wangari alikuwa amekwenda kuweka gari yake mafuta ndipo alipoamua kuingia msalani kujisaidia.

Alisema baada ya Wangari kumaliza kujisaidia alisikia mtu akitembea nyuma ya choo alichokuwepo na hapo ndipo alipogundua kuwa mshtakiwa alikuwa ameweka simu kwenye dirisha la choo hicho na kumrekodi.

Kutokana na hali hiyo Wangari aliwaeleza wafanyakazi wengine wa kituo hicho waliokuwa pale kuhusu kilichomtokea na ndipo kesi ikaripotiwa polisi na mtuhumiwa kukamatwa.

Mwendesha mashtaka alipendekeza picha za CCTV zitumike kama ushahidi kwenye kesi hiyo lakini Hakimu akaamuru zisitumike.

Aidha, Hakimu huyo aliahirisha kesi hiyo hadi tarehe mosi Novemba mwaka huu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

Hospitali za China zilifurika wagonjwa, wazee kipindi cha wa likizo ya Mwaka Mpya wa Lunar

Spread the loveHOSPITALI  nchini China zimejaa wagonjwa na wazee katika kipindi cha...

Kimataifa

Papa Francis ayataka mataifa ya nje kuacha kupora mali DRC

Spread the love  KIONGOZI wa kanisa Katoliki Papa Francis, ameyataka mataifa ya...

Kimataifa

Mashabiki wakabiliwa na mashtaka ya mauaji baada ya wafuasi wa Arsenal na Manchester City kupigana Uganda

Spread the love  MASHABIKI wawili wa soka nchini Uganda wanakabiliwa na mashtaka...

Kimataifa

China inatathmini upya sera za wafanyakazi

Spread the love  WAKATI idadi ya watu wa nchi China inapungua, Beijing...

error: Content is protected !!