Friday , 29 March 2024
Home Kitengo Michezo Kocha Yanga ang’aka kutumika wachezaji nane wa kigeni mchezo mmoja.
Michezo

Kocha Yanga ang’aka kutumika wachezaji nane wa kigeni mchezo mmoja.

Nasriddine Nabi, Kocha wa Yanga (katikati)
Spread the love

 

KOCHA mkuu wa klabu ya Yanga, Mohmed Nabi ameonekana mbogo, kutokana na kanuni ya kutumia wachezaji nane wakigeni katika mchezo mmoja, kitu kinachoonekana kumumiza. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Nabi ameyasema hayo jana tarehe 18 Oktoba, 2021 kwenye mkutano na waandishi wa habari, kuelekea mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Kmc utakaopigwa kwenye Uwanja wa Majimaji Songea.

Kocha huyo ameshangazwa kuwa, msimu uliopita waliruhusiwa kuchezesha wachezaji wote 10 wa kigeni waliokuwa wamesajiriwa na timu husika, lakini kwa msimu huu imekuwa tofauti na uamuzi huo umekuja wakati dirisha hilo la usajili limeshafungwa.

“Mwaka jana walikuwa wanaruhusu wachezaji 10, lakini sasa hivi wanaruhusu nane na wamefanya hivyo wakati dirisha lilishafungwa.”

“Umejiandaa kuwachezasha wachezaji 10 na umewalipia kila kitu, na sheria inakuja eti unatakiwa kuchezesha wachezaji nane, hiyo inatuumiza kutokana na mipango kuingiliana.” Alizungumza Nabi

Toka kuanza kwa msimu huu, kanuni ya usajili wachezaji wa kigeni ilibadilika kutoka 10 na kuongezwa hadi kufikia 12, lakini kwenye kila mchezo wanatakiwa wachezaji nane tu, kuwa sehemu ya mechi.

Aidha Nabi aliendelea kusema kuwa, kutokana na sharia hiyo inawalazimisha kuwaweka nje baadhi ya wachezaji sio tu wanakiwango kibovu, bali kukidhi matakwa ya sheria.

Sisi tunawachezaji 10 kuna wengine wanazidi ya hao, na ndio kusema kila mechi kuna wachezaji wawili hawatocheza na sio kwa sababu wanakiwango kibovu hapana, bali sheria zinabana, tungejua tungesajiri nane tu, ili tusilete usumbufu.” Alikazia Nabi

Katika hatua nyingine klabu hiyo hii leo, itashuka Uwanjani kwenye muendelezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, ambapo majira ya saa 1o itamenyana na Kmc kutoka Manispaa ya Kinondoni, Jijini Dar es Salaam ambao ndio wenyeji wa mchezo huo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Makala & UchambuziMichezo

TFF kuamua hatima ya Amrouche

Spread the loveHATIMA ya Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Adel Amrouche kuendelea...

Habari za SiasaMichezo

Matinyi: Dk. Ndumbaro alifanya utani ukaguzi mechi za Yanga, Simba

Spread the loveMsemaji Mkuu wa Serikali, Mobhare Matinyi amesema kauli iliyotolewa na...

Michezo

Gethsemane Group Kinondoni (GGK) waachia video ya Bwana Wastahili

Spread the loveWAIMBAJI maarufu nchini kutoka Gethsemane Group Kinondoni (GGK)SDA wameachia video...

BiasharaMichezo

Gamondi kocha bora mwezi Februari, NBC yamjaza manoti

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) ambae ni mdhamini Mkuu...

error: Content is protected !!