January 17, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Simba yaitisha mkutano mkuu

Spread the love

KLABU ya soka ya Simba kupitia bodi ya wakurugenzi, imeitisha mkutano mkuu wa mwaka ambao utafanyika Tarehe 21, Novemba 2021 kwenye ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Julius Nyerere. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Mkutano huo unaitishwa kwa mujibu wa ibara ya 21 (1), ya katiba ya klabu hiyo ambayo ilifanyiwa marekebisho mwaka 2016, kwa kuruhusu mfumo wa mabadiliko ya uwendeshaji wa klabu hiyo.

Katika taarifa iliyotolewa kupitia page mbalimbali za mitandao ya kijamii ya klabu hiyo, imeeleza kuwa Ajenda za mkutano huo zitasambazwa kwa wanachama siku saba kabla ya mkutano huo kupitia matawi yao, kama ilivyoainishwa kwenye ibara ya 21(2) ya klatiba yao.

Mkutano huo utaanza majira ya saa tatu asubuhi, kwa wanachama mbalimbali wa klabu hiyo kuhudhulia.

Mara ya mwisho Simba kufanya mkutano mkuu wa mwaka, ilikuwa tarehe 7 Februari 2021, ambapo moja ya ajenda ilikuwa kufanya uchaguzi wa kuziba nafasi ya mwenyekiti na Murtaza Mangungu alifanikiwa kushinda nafasio hiyo iliyoacha wazi na Swedy Nkwabi ambaye alijiuzuru.

Mangungu alishinda kiti hiko mara baada ya kumshinda mpinzani wake, Juma Nkamia kwa kupata kura 802, kati ya kura 1140 zilizopigwa na wanachama waliojitokeza kwenye mkutano huo.

 

 

error: Content is protected !!