March 1, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Amnesty International: Burundi si shwari

Mji wa Bujumbura

Spread the love

SHIRIKA la Kimataifa la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limetoa ripoti inayoonyesha hali ya usalama kutokuwa shwari nchini Burundi, anaandika Mwandishi Wetu.

Taarifa ya Shirika hilo imesema kwamba nchi hiyo imekuwa ikikabiliwa na vitendo vya mateso, watu kufungwa bila makosa, kubakwa na hata kuuwawa.

Shirika hilo limetoa tahadhari kwa umoja wa mataifa kufikiria kwa kina kuhuzu wakimbizi wanaorejea Burundi kutoka Tanzania kwa kuwa wengi wapo katika hatari za kiusalama nchini mwao.

Mwezi uliopita, Tanzania, Burundi na Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia wakimbizi (UNHCR) walikubaliana kwamba kufikia mwisho wa mwaka huu wawe wamewarejesha wakimbizi 12,000 wanaoishi Tanzania wanaotaka kurudi kwao kwa hiari.

Shirika la Amnesty International linasema, mpango huu unahatarisha maisha ya maelfu ya wakimbizi na linaamini kuwa wakimbizi wengi wanarejeshwa nyumbani kwao kutokana na msukumo wa ushawishi kutoka serikali ya Tanzania na Burundi.

error: Content is protected !!