Tuesday , 27 February 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Sauti ya kiongozi wa IS yazusha taharuki
Kimataifa

Sauti ya kiongozi wa IS yazusha taharuki

Abu Bakr al-Baghdadi
Spread the love

WANAMGAMBO wa Islamic State wametoa kanda ya sauti ya kiongozi wa kundi hilo, Abu Bakr al-Baghdadi, anaandika Mwandishi Wetu.

Mzungumzaji aliye na sauti kama ya kiongozi huyo wa IS anasikika akitaja tishio la hivi karibuni la Korea kaskazini dhidi ya Japan na Marekani.

Anazungumzia pia vita vya kupigania ngome za IS kama Mosul, mji uliodhibitiwa upya na vikosi vya Iraq mwezi Julai.
Baghdadi, ambaye anasakwa hajaonekana mbele ya umma tangu Julai 2014 jambo lililozusha uvumi mkubwa kuhusu hatma yake.

Mara ya mwisho alipoonekana alikuwa anatoa hotuba katika mskiti mkubwa wa al Nuri mjini Mosul baada ya IS kuudhibiti mji huo na kulitangaza kuwa eneo wanalo litawala.

Aliopulizwa kuhusu kanda hiyo ya sauti, msemaji wa vikosi vya Marekani vinavyopigana na IS, Ryan Dillon, amesema “pasi kuwepo ushahidi wa kuthibitishwa wa kifo chake, tumeendelea kuamini kwamba yuko hai”.

Msemaji wa idara ya ulinzi ameiambia BBC: “tunahafahamu kuhusu kanda hiyo ya sauti inayodaiwa kuwa ya Abu Bakr Al-Baghdadi na tunachukua hatua kuikagua.

Wakati huu hatuna sababu ya kuwa na shaka ya uhalisia wake, na hatuwezi kuithibitisha kwa hivi sasa.”

Kundi la wanamgambo wa kiislamu IS, linatambulika kwa ghasia dhidi ya raia na wafungwa, limesukumwa nyuma Iraq na Syria mwaka huu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

Wanajeshi Ukraine waishiwa risasi, 31,000 wauawa

Spread the loveRais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy amesema zaidi ya wanajeshi 31,000...

Kimataifa

Waziri mkuu Palestina ajiuzulu

Spread the loveWaziri Mkuu wa Palestina, Mohammed Shtayyeh ametangaza kujiuzulu pamoja na...

Kimataifa

Rais mstaafu ahukumiwa miaka 4 jela

Spread the loveMahakama ya mjini Tunis imemhukumu rais wa zamani wa Tunisia,...

Kimataifa

Malawi yaondoa vikwazo vya viza kwa nchi 79 ikiwamo TZ

Spread the loveWaziri wa usalama wa ndani nchini Malawi, Ken Zikhałe ametangaza...

error: Content is protected !!