February 28, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Serikali ya Magufuli yalitia ‘kitanzi’ Raia Mwema

Dk. Hassan Abbas, Mkurugenzi wa Idara Habari Maelezo. Picha ndogo toleo la gazeti Raia Mwema lililosababisha kufungiwa

Spread the love

UHURU wa vyombo vya habari hususani magazeti umezidi   kuwa mashakani baada ya leo serikali kutangaza kulifungia gazeti linalotolewa kilawiki la Raia mwema, anaandika Faki Sosi.

Gazeti hilo lilianzishwa na kumilikiwa na waandishi wa habari wakongwe na jana limefungiwa katika kipindi cha miezi mitatu.

Kufungwa kwa gazeti hilo kumekuja ikiwa imepita wiki moja tangu serikali ilipolifunga gazeti la MwanaHALISI linalomikiwa pia na Mwandishi,  Saed Kubenea.

Mkuregenzi wa Idara ya Habari (Maelezo), Dk.  Hassan Abbas ambaye pia ndiye msemaji wa Serikali leo ametangaza kulifungia gazeti hilo kwa  muda wa siku 90.

Wakati Rais Mwema likifungiwa miezi mitatu, MwanaHALISI limefungiwa miezi 24 miaka (miwili).

Mhariri wa gazeti hilo jana aliitwa na serikali kujieleza kwa nini alifungiwe kwa madi ya kuandika habari ya uchambuzi iliyobebwa na kichwa cha habari,  “Magufuli urais utamshinda”

Habari hiyo ilichapishwa katika gazeti hilo la Septemba 27 mwaka huu. Mhariri mtendaji wa gazeti hilo, Godfrey Dilunga amethibitisha kufungiwa.

error: Content is protected !!