Saturday , 27 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Aliyemchapa kofi Rais Macron hadharani miezi 4 jela
Kimataifa

Aliyemchapa kofi Rais Macron hadharani miezi 4 jela

Spread the love

 

DAMIEN Tarel, amehukumiwa kifungo cha miezi minne jela, kwa kosa la kumpiga kofi Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron, hadharani. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Jana Alhamisi tarehe 10 Juni 2021, Mahakama ya Ufaransa, ilimhukumu Tarel kwenda jela miezi 18, baada ya kumkuta na hatia katika shtaka la shambulio dhidi ya afisa wa umma.

Mwendesha mashtaka wa mahakama hiyo, alitoa hukumu hiyo akisema kitendo kilichofanywa na Tarel hakikubaliki, kwa kuwa ni kitendo cha kuzua ghasia kwa makusudi.

Tukio hilo lililotikisa dunia, lilitokea tarehe 8 Juni 2021, katika ziara ya Rais Macron kwenye Shule ya Hoteli iliyoko kwenye Mji wa Tain-I’Hermitage, mkoani Drom, nje ya Jiji la Valance, nchini Ufaransa.

Rais Macron alikumbwa na kadhia hiyo, wakati akiwasalimia wananchi waliojitokeza katika ziara yake, na kwamba alipofika karibu na Tarel, raia huyo alimpiga kofi la shavuni.

Baada ya kufanya tukio hilo, Tarel aliwekwa kizuizini tangu Jumanne hadi jana, alipohukumiwa kutumikia kifungo cha miezi minne jela.

Hata hivyo, mfungwa huyo anaonekana kutojutia kitendo alichokifanya kwani, alidhamiria kutenda kosa hilo, kabla ya Rais Macron kuzuru katika mkoa huo, akipinga sera zake.

Tarel aliiambia mahakama kwamba, uamuzi wa kumpiga kofi kiongozi huyo wa Ufaransa aliuchukua dakika za mwisho, kwa kuwa awali alipanga kumrushia yai au Ice Cream.

Raia huyo wa Ufaransa aliieleza mahakama hiyo kuwa, Rais Macron anaiharibu nchi hiyo.

Tarel amepunguziwa kifungo hicho, kwani hukumu ya shtaka alilofunguliwa ni miaka mitatu jela na faini ya Euro 45,000.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

Habari MchanganyikoKimataifa

Tetemeko la ardhi laua 7, lajeruhi 800 Taiwan

Spread the loveWatu wapatao saba wamefariki dunia na wengine zaidi ya 800...

error: Content is protected !!