May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kubenea amchukulia fomu Allly Saleh ‘Alberto’

Spread the love

ALIYEKUWA Mbunge wa jimbo la Ubungo Saed Kubenea jana alijitokeza kwenye makao makuu ya Shirikisho la Mpira Tanzania (TFF) kumchukulia fomu ya nafasi ya Urais Ally Saleh ‘Alberto’ na kutimiza idadi ya watia nia 10 walijitokeza kwenye mchakato huo. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Uchaguzi huo ambao utafanyika tarehe 7 Agosti, 2021 Jijini Tanga ambao utakuwa na jumla ya wapiga kura 83, ambao wamepunguzwa kutoka 129 mara baada ya kufanyika mabadiliko ya katiba mwaka 2019.

Kubenea alifika majira ya saa 7:45 mchana, na kufanikiwa kuchukua fomu hiyo na kusema kuwa ameamua kumchukulia fomu Ally saleh kutokana na kuchelewa kufika Dar es Salaam akitokea visiwani Zanzibar ambapo ndio makazi yake.

Ally Saleh ‘Alberto’

Alisema “Nimefika kwenye ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), kuja kuchukua fomu ya Urais kwa niaba ya Ally Saleh ‘Alberto’ aishie Zanzibar, amenituma nije kumchukulia fomu amechelewa kufika Dar es Salaam, yupo njiani kwenye boti na hatimaye fomu nimepewa baada ya mizengwe.”

Aidha Kubenea ambaye ni wakilishi wa mgombea huyoa aliongezea kuwa nia ya aLLY salehe kugombania nafasi hiyo ni kupigania maslai ya Mpira wa Zanzibar ili ipate uwakilishi kwenye Shirikisho la Mpira wa Miguu Dunia (FIFA).

“Tff ni chama cha mpira wa miguu Tanzania japokuwa ni cha Tanzania bara, laikini kinasimamia mpira mpaka visiwani, Zanzibar wanakero ya muda mrefu kwa ZFA zfa kutokuwa mwanachama wa fifa na wanaamini timu TFF inawawekea uzibe kwa hiyo.”Alisema Mwakilishi huyo

“Anataka kugombea Urais wa TFF ili aisaidie Zanzibar kupata uwanachama wa FIFA na kukuza mpira wa Miguu nchini.”Aliongezea Kubenea

error: Content is protected !!