Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rais wa Botswana aondoka Tanzania, Balozi Mulamula atoa neno
Habari za Siasa

Rais wa Botswana aondoka Tanzania, Balozi Mulamula atoa neno

Spread the love

 

RAIS wa Botswana, Mokgweetsi Masisi, amehitimisha ziara ya kikazi ya siku mbili nchini Tanzania na kuondoka kurejea nchini mwake. Anaripoti Nasra Bakari, DMC … (endelea).

Masisi ameondoka leo Ijumaa, tarehe 11 Juni 2021, saa 5 asubuhi, katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam-Tanzania, mara baada ya kumaliza ziara hiyo, aliyoianza jana Alhamisi, kwa mwaliko wa Rais Samia Suluhu Hassan.

Katika Uwanja wa Ndege, Rais Masisi, amesindikizwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania, Balozi Liberata Mulamula ambaye pia alimpokea alipowasili nchini humo.

Akizungumzia ziara hiyo, Balozi Mulamula amesema, licha ya Botswana kuwa nchi ndogo “lakini ni tajiri katika madini na mifugo na katika ziara hii, tutafungua milango zaidi kwa wawekezaji.”

“Imekuwa ziara fupi, lakini yenye mafanikio sana na amefurahi kukutana na Rais Samia,” amesema

Balozi Mulamula amesema, “Diplomasia ya Uchumi chini ya Rais Samia imeendelea kuimarika. Tufungue milango zaidi na hii ilikuwa ziara ya kiuchumi zaidi na si ya kisiasa.”

Kuhusu maagizo ya Rais Samia ya kuwataka mawaziri na wataalam wa Tanzania na Botswana kufufua kamati ya kudumu ya pamoja (JPC) ambayo haijakutana tangu mwaka 2009, Balozi Mulamula amesema, watalifanyia kazi agizo hilo kwa maslahi mapana ya mataifa hayo.

“Tume ya pamoja inaangalia sekta mbalimbali kama ya biashara, madini, nishati na maeneo mengine mengi, hii ndiyo inaimalisha ushirikiano mkubwa katika kukuza biashara,” amesema Balozi Mulamula

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

error: Content is protected !!