Saturday , 2 December 2023
Home Habari Mchanganyiko Afya ya akili yatajwa chanzo kuvunjika ndoa
Habari MchanganyikoTangulizi

Afya ya akili yatajwa chanzo kuvunjika ndoa

Spread the love

CHANGAMOTO ya afya ya akili, imetajwa kuwa chanzo cha migogoro inayopelekea ndoa nyingi kuvunjika. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma…(endelea).

Hayo yamebainishwa leo tarehe 28 Septemba 2023, jijini Dodoma na Kaimu Mufti Mkuu, Sheikh Ally Ngeruka, akielezwa utafiti uliofanyika kubaini sababu za ndoa nyingi kuvunjika ndani ya muda mfupi baada ya kufungwa.

Sheikh Ngeruka amesema baadhi ya watu hufunga ndoa na wenzao wao bila kujua kama wanachangamoto ya akili, kitendo kinachopeleka kuwabaini baada ya kuingia kwneye ndoa kutokana na vitendo visisvyo vya kawaida wanavayofanya.

“Wakasema jamii haijajua changamoto ya afya ya akili, MTU anamuona mwenzake amevaa suruali nzuri naye amevaa gauni zuri anadhani kwamba yuko sawa baada ya hapo wanaanza mahusisno hatimaye zinafanyika ndoa kutokana na changamoto ya akili hawakai ndoa imekufa, wengine mwezi mmoja, mwaka mnajua chanzo ni Nini? Ni afya ya akili,” amesema Sheikh Ngeruka.

Kiongozi huyo wa dini amesema tatizo la afya ya akili ni janga kama yalivyokuwa magonjwa mengine ikiwemo Ugonjwa wa Virusi vya Korona ulioibuka 2019 (COVID-19).

“Kuna changamoto ya afya ya akili katika jamii zetu, kama vile tulivyokuwa na COVID-19, Ebola na maradhi mengine mengi, lakini  sasa kuna tatizo la afya ya akili. Tulipata bahati ya kuzungumza na mkurugenzi wa Hospitali ya Mirembe, ikafika mahaki akaeleza uzito wa tatizo hili kwneye jamii, aligusia namna gani ndoa za sasa zinavyovuruguka kwa muda mchache,” amesema Sheikh Ngeruka.

Sheikh Mruma ameitaka Serikali na jamii kiujumla, watafute suluhu ya tatizo hilo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari Mchanganyiko

GGML waungana na Biteko kuanika mbinu za mapambano dhidi ya Ukimwi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari MchanganyikoTangulizi

Mwalimu jela miaka mitatu kwa rushwa

Spread the loveMAHAKAMA ya Hakimu Mfawidhi, wilaya ya Igunga, mkoani Tabora imemhukumu...

Habari Mchanganyiko

Waziri Bashungwa aagiza wahandisi kujengewa uwezo

Spread the loveWAZIRI wa Ujenzi, Innocent Bashungwa ameiagiza Bodi ya Usajili wa...

Habari Mchanganyiko

Heche ataka mawakili vijana kuamka sakata Mpoki

Spread the loveMWENYEKITI wa Mawakili Vijana Tanzania kutoka Chama cha Mawakili wa...

error: Content is protected !!