MFANYABIASHARA maarufu nchini, Azzim Dewji, ameitaka Serikali iwachukulie hatua wezi wa fedha za umma, akisema kitendo cha kuwaacha huru kinawaibua wengine. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma… (endelea).
Dewji ametoa wito huo leo tarehe 28 Septemba 2023, katika Baraza la Maulid ya Mtume Muhammad, yaliyofanyiwa jijini Dodoma.
Aidha, Dewji ameipongeza Serikali ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, kwa kuendelea kuimarisha maendeleo ya nchi.
“Tunawaona mkizunguka nchi nzima kufanya kazi, mkiondoka vibaka wao wanafungua droo wanaiba hela. Naomba muwashughulikie msipowashughulikia wataongezeka kila siku,” amesema Dewji.
Nakuuliza.
Je, wewe siyo kibaka unataka kumyang’anya mjane mzawa kiwanja chake na kutaka kujificha kwenye kichochoro cha Mahakama kwa nguvu za pesa zako?