Thursday , 2 May 2024
Home Habari Mchanganyiko ACT Wazalendo: Tunafanya kazi kuhakikisha Z’bar inakuwa na uchaguzi bora
Habari Mchanganyiko

ACT Wazalendo: Tunafanya kazi kuhakikisha Z’bar inakuwa na uchaguzi bora

Spread the love

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha ACT- Wazalendo Zanzibar Othman Masoud Othman, amesema wanafanya kazi kubwa, ili Zanzibar iwe na mazingira bora ya uchaguzi wa kidemokrasia na kuwezesha kuzuia matatizo ya uvunjifu wa amani wakati wa uchaguzi. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea)

Othman ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, ameyasema hayo leo tarehe 24 Julai, 2022 huko Tunguu wilaya ya Kati Unguja baada ya kufungua ofisi za chama hicho Jimbo la Tunguu Mkoa wa Kati Kichama.

Alisema kwa kuzingatia uzalendo na nia na njema ya kujiunga na Serikali ya Umoja wa Kitaifa,  chama hicho kupitia viongozi  wake kimekuwa kikishiriki  vyema katika kikosi kazi cha kutoa mapendekezo kuhusu uundwaji wa Katiba mpya ya Tanzania na kwamba kimewasilisha maoni yake kwa maandishi juu ya mambo muhimu yanayopaswa kuzingatiwa katika suala hilo.

Alisema suala hilo limekuwa likifanywa kwa kuzingatia uzalendo mkubwa unaofanywa na viongozi  wa ngazi tofauti kwa nia ya kuhakikisha kwamba Taifa linajenga mazingira bora ya uchaguzi wa kidemokrasia na amani ya kweli.

Kuhusu suala la Serikali ya Umoja wa Kitaifa , alisema, viongozi waliomo Serikali wanajitahidi kuhakikisha kwamba wanatimiza wajibu wa majukumu ya waliopewa kwa kuwa wamekula kiapo cha kuwatumika wananchi kwa uadilifu na utiifu mkubwa.

Amemewataka wananchi kuendelea kushirikiana na viongozi katika kujenga nchi kwa  kuunga mkono jitihada za viongozi mbali mbali katika kuhakikisha wanatimiza vyema wajibu waliopewa wa kuitumika ipasavyo nchi yao.

Kuhusu kauli za ukosoaji kwa viongozi zinazotolewa na chama hicho, Othman alisema kufanya hivyo ni kutekeleza wajibu wa kuisaidia nchi ili iweze kuwatumikia vyema wananchi kwa uzalendo na taifa liweze kupiga hatua  za kimaendeleo kwa kasi zaidi.

Akizungumzia suala la Sensa ya Watu na Makaazi, amewataka wanachama wa chama hicho na wananchi kwa jumla kuhakikisha kwamba wote wanashiriki kuhesabiwa kwa kutoa mashirikiano ipasavyo siku itakapowadia.

Alisema kwamba sensa ni jambo muhimu litakalowezesha taifa kupata takwimu na tarifa sahihi za aina mbali mbali na kusaidia serikali kuweza kupanga mipango mbali mbali ya maendeleo kwa kutumia matokeo ya taarifa zitakazopatikana kwenye sensa.

Naye Naibu Katibu Mkuu wa Chama hicho Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui ambaye pia ni Waziri wa Afya Zanzibar, alisema viongozi wa chama hicho wataendelea kutekeleza majukumu ya kiserikali waliyopewa kwa uzalendo mkubwa ili kusaidia jitihada za unjenzi wa nchi kupitia Serikali ya Umoja wa Kitaifa.

Mapema, Mwanasheria Mkuu wa Chama hicho ambaye pia ni Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar Omar Said Shaaban, alisema pamoja na majukumu ya kiserikali waliyopowa pia viongozi wa chama hicho wataendelea na jitihada za kukiimarisha chama.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yashiriki maadhimisho Mei Mosi Arusha

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeungana na maelfu ya...

Habari Mchanganyiko

Makonda autaka mgodi kubadilisha maisha ya wana-Geita

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda ametoa wito kwa...

Habari MchanganyikoMakala & Uchambuzi

Je, miji ya Uingereza inafilisika?

Spread the loveMNAMO 1890, mwandishi mmoja wa habari Mmarekani aitwaye Julian Ralph...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Equity Bank yaendelea kusotea mabilioni ya fedha mahakama rufani

Spread the loveBENKI za Equity ya Tanzania na Kenya, zimeendelea kupambana mahakamani...

error: Content is protected !!