MWENYEKITI wa Kamati ya Kitaifa ya Maaskofu na Mashehe ya Maadili, Amani na Haki za Binadamu kwa jamii ya Madhehebu nchini Askofu William Mwamalanga amempongeza Mkuu Mpya wa Jeshi la Polisi (IGP), Camilius Wambura huku akimtaka awafute kazi askari wanaokiuka haki za raia. Anaripoti Mwandishi Wetu… (endelea).
Askofu Mwamalanga ameyasema hayo kwenye taarifa aliyotoa kwa vyombo vya habari siku chache baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kumteua kuwa IGP akichukua nafasi ya IGP Simon Sirro ambaye ameteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Zimbambwe.
“Sisi viongozi wa dini tunamshauri IGP Wambura kulijenga jeshi litakalo kumbatia raia mwema badala ya kuyakumbatia magenge ya rushwa, vigogo wa dawa za kulevya, majambazi, waongo na vigogo wa Serikali wanaofisadi mali za umma raia wema ndiyo silaha muhimu kwa polisi kutokomeza wahalifu kuliko ilivyo sasa hivi,” alisema.
Askofu Mwamalinga alisema duniani kote mataifa yanayofanikiwa , mchango mkubwa unachangiwa na jeshi la polisi, hivyo imani yao ni kuona chombo hicho kinachochea maendeleo ya jamii.
Alisema iwapo jeshi hilo litakumbatia raia wema na taifa litakuwa na jamii yenye uadilifu na kupenda amani kuliko kuwa na polisi wanaowafundisha wahalifu mbinu za uhalifu.
Aidha Askofu Mwamalanga amemkumbusha IGP Wambura kuwa amani ni msingi wa haki na kumuomba atembelee vituo vyote vya polisi nchini ili ajionea uvunjifu mkubwa wa haki za raia wema wakiwamo askari polisi wa vyeo vya chini ambao huwekwa lokapu na wakubwa zao bila sababu za msingi.
Mwamalanga alimuomba IGP Wambura kuhakikisha anatengeneza jeshi ambalo litafuata misingi ya jeshi hilo na sio kujihusisha na siasa hali ambayo inashusha heshima ya jeshi hilo.
“Tunataka kuona jeshi ambalo litafuata PGO katika kutekeleza majukumu yake na sio maagizo ya viongozi wa kisiasa, kwani asilimia kubwa yanaumiza wananchi,” alisema.
Ni Vizuri Raia, Wajenge Urafiki na Askali Wanaowalinda! Ukimuona Police Uone Amani Furaha, Uamini Huko Salama! Sio Kumuona Police, Ukaona ni Adui Mkubwa Kuliko Huyo Mkosaji! Asante Saana Bishop Mwamaranga! Nafikili Hii Itafika Mahali Husika!