Friday , 19 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Rais Samia aonya bodaboda wizi wa ukwapuaji
Habari Mchanganyiko

Rais Samia aonya bodaboda wizi wa ukwapuaji

Waendesha pikipiki (Bodaboda) wakiwa maeneo ya mjini katika shughuli zao za kawaida
Spread the love

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amewataka wasafirishaji wanaotumia pikipiki maarufu kama bodaboda nchini humo kuachana na vitendo vya wizi wa ukwapuaji na kushiriki vitendo vya ujambazi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma…(endelea)

Mkuu huyo wa nchi ametoa wito huo leo Jumamosi tarehe 24 Julai, 2022, akizungumza nao kwa njia ya simu wakati wa kongamano la kuimarisha ushiriki wa madereva wa bodaboba na bajaji katika sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022.

“Ninyi ni maafisa usafirishaji wa Taifa lakini baadhi yenu wanawaharibia sifa yenu kwa kutumika kukwapua na kuiba mizigo ya watu lakini kutumika kwa ujambazi, niwaombe sana jilindeni msipoteze sifa yenu ninyi ni watu muhimu sana kwenye Taifa letu,” amesema Rais Samia.

Ameongeza kuwa bodaboda ni watu muhimu kwa kile alichoeleza kuwa ndiyo wasafirishaji wa wanyonge kwani gharama zao ni za chini.

“Tunapozungumzia usafiri wa wanyonge huo ndio usafiri wetu wanyonge ambao mnaweza kusafirisha watu kwa bei nafuu,” ameongeza.

Rais pia ameonesha kutambua uwepo wa wasomi katika kundi hilo na kuahidi kuzifanyia kazi changamoto zote watakazoeleza katika kongamano hilo.

Sekta yenu ni muhimu na najua kati yenu kuna wasomi wamo humo ndani, wenye diploma, wenye certificate (cheti), wenye shahada zao, niwaambie tu kwamba mama yenu nipo pamoja na ninyi, changamoto zote mtakazozungumza leo Mkuu wa Mkoa ataniletea ili tuzifanyie kazi,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

Habari Mchanganyiko

Carbon First, Ruangwa wasaini makubaliano ya biashara ya hewa ukaa

Spread the love  KAMPUNI ya Carbon First Tanzania Limited na Halmashauri ya...

Habari Mchanganyiko

CBE yawakumbuka wenye mahitaji maalum Jangwani

Spread the loveCHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimetoa msaada mbalimbali na...

Habari Mchanganyiko

Mume auwa mke kwa kumchoma visu, ajisalimisha Polisi

Spread the loveJACKSON Kalamji (49), anashikiliwa na Jeshi la Polisi jijini Mwanza,...

error: Content is protected !!