July 3, 2022

Uhuru hauna Mipaka

ACT-Wazalendo yawakaribisha Mdee na wenzake

Spread the love

CHAMA cha ACT-Wazalendo kimewafungua milango na kuwakaribisha Halima Mdee na wenzake 18 waliotimuliwa katika Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), watakapowiwa kujiunga na chama hicho. Anaripoti Faki Ubwa, Dar es Salaam … (endelea).

Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa chama hicho, Ado Shaibu jana tarehe 25 Mei 2022 jijini Dar es Salaam.

Shaibu ambaye alikuwa mgeni rasmi katika uchaguzi wa viongozi wa chama hicho ngazi ya jimbo la Kawe, amesema Mdee na wenzake ni wanasiasa waliouaminisha umma kuwa mwanamke anaweza kusimama mwenyewe kwenye uchaguzi na kutwaa kiti cha ubunge.

Amesema wanasiasa hao wameondoa dhana ya kuwa wanawake wanaojihusisha na siasa ni wale wanategemea uteuzi wa viti maalam pekee.

Amesema Mdee na wenzanke ni kielelezo cha wanawake wapambanaji “kwenye ukweli lazima usemwe Halima Mdee na wenzake licha ya changamoto zote ni kielelezo cha mafanikio makubwa ya wanawake kwenye nchi ya kujenga uongozi kati vyama vya siasa.

“Tupende tusipende Mdee na wenzake ni kielelezo cha mafanikio ya wanasiasa wanawake nchini Tanzania.

“Ni kielelezo cha wanawake ambao wapo tayari kulala ndani muda wowote… wamefikia kwenye rekodi ya juu ya kuwa wanawake wanasiasa nchini kwa sifa hizo nilizosema nitakuwa mtu wa mwisho kusema wasikaribishwe ACT’’ amesema Ado.

Ado amewataka wanachama wa ACT Wazalendo jimboni humo kunyoosha mkono juu kama wapo tayari kuwakaribisha wanasiasa hao ukumbi nzima ulinyoosha mikono.

Ado Shaibu, Katibu Mkuu ACT-Wazalendo

Tarehe 27 Novemba 2020, Chadema kupitia Kamati kuu kiliazimia kuwafukuzwa Mdee na wenzake 18 kwa madai ya kukiuka Katiba na kanuni za chama hicho kwa uamuzi wao wa kwenda bungeni kuapa na kuwa wabunge wa viti maalum bila kupitishwa na chama hicho.

Wabunge hao ni pamoja na Mdee, Esther Matiko, Grace Tendega, Cecilia Pareso, Ester Bulaya, Agnesta Lambart, Nusrati Hanje, Jesca Kishoa na Hawa Mwaifunga.

Wengine ni Tunza Malapo, Asia Mohammed, Felister Njau, Nagenjwa Kaboyoka, Sophia Mwakagenda, Kunti Majala, Stella Fiao, Anatropia Theonest, Salome Makamba na Conchesta Rwamlaza.

error: Content is protected !!