Saturday , 4 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Msajili wa vyama ampiga ‘Stop’ Mbatia NCCR-Mageuzi
Habari za SiasaTangulizi

Msajili wa vyama ampiga ‘Stop’ Mbatia NCCR-Mageuzi

James Mbatia
Spread the love

 

NAIBU Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Sisty Nyahoza, amemtaka aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi na wajumbe wa sekretarieti yake iliyovunjwa, kuacha kujihusisha na shughuli za kisiasa za chama hicho, kwa kuwa wamevuliwa nyadhifa zao.Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Akizungumza na wanahabari leo Jumatano, tarehe 25 Mei 2022, jijini Dar es Salaam, Nyahoza amedai, kitendo cha mtu kufanya siasa kwa jina la chama ambacho siyo kiongozi ni kosa la jinai.

Naibu Msajili huyo wa vyama vya siasa, ametoa marufuku hayo akitangaza msimamo wa ofisi yake kuhusu maamuzi ya kikao cha Halmashauri Kuu ya NCCR-Mageuzi, kilichofanyika Jumamosi iliyopita, ya kumsimamisha uenyekiti Mbatia na sekretarieti yake.

 

Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa, Sixty Nyahoza,

“Kwa mujibu wa kifungu cha 8B cha Sheria ya Vyama vya Siasa, ni kosa kwa mtu yeyote kufanya shughuli za siasa kwa jina la chama ambacho yeye siyo kiongozi. Kufanya kitendo hjcho ni kosa la jinai,” imesema taarifa ya Nyahoza.

Taarifa hiyo imesema “hivyo ninawaasa Mbatia, Angelina John Mutahiwa, Anthony Komi na wanachama wengine wa NCCR-Mageuzi waliokiwa wajumbe wa Sekretarieti iliyovunjea tarehe 21 Mei 2022, kutojifanya ni viongozi kwani kufanya hivyo ni kosa la jinai.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Sabaya afutiwa kesi, ruksa kugombea uongozi

Spread the loveMwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali DPP leo Ijumaa amefuta rufaa...

Habari za Siasa

Serikali yasaka bilioni 3 kujenga daraja Mto Mpiji

Spread the loveSerikali imesema inaendelea na juhudi za kutafuta fedha kiasi cha...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kwafukuta kisa chaguzi, Lissu aibua tuhuma nzito

Spread the loveCHAGUZI za kusaka viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo...

Habari MchanganyikoTangulizi

Kimbunga “HIDAYA” chaendelea kuimarika, wananchi wapewa tahadhari

Spread the loveMAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) inaendelea kutoa taarifa...

error: Content is protected !!