
Wavuvi wakiwa wameegesha mitumbwi yao baada ya kutoka kuvua samani baharini
MBUNGE wa Viti Maalum Wanawake Mkoa wa Dodoma (CCM), Mariam Ditopile ameitaka Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi kuja na mipango kabambe ambayo itaboresha sekta hiyo ili iweze kuzalisha ajira kwa wingi kama ilivyokua miaka ya nyuma. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma…(endelea).
Ditopile ametoa kauli hiyo leo Jumatano, tarehe 25 Mei 2022 wakati akichangia Bajeti ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi ya mwaka 2022/23 Bungeni jijini Dodoma.
“Mwaka 2014/15 Tanzania tulia tunatoa tani zaidi ya 45,000 ya minofu ya Sangara na mazao yake,lakini mwaka 2021 tumetoa tani 41,000 tu, Niwe mkweli hali ya Sangara katika Ziwa Viktoria imekua mbaya Sana sijui kama Waziri hili jambo mmeliona na kulitafutia ufumbuzi,” amesema
Amesem, ukienda kuwahoji wanachinga wa Mikoa ya Kanda ya Ziwa wengi walikua waajiriwa katika Viwanda vinavyochakata mazao ya Uvuvi, Viwanda hivyo kwa sasa vimepunguza uzalishaji tukumbuke mapato yaliyokua yanapatikana kupitia Sangara yaliyokua yanaleta maendeleo nchini.

Amemtaka Waziri wa Uvuvi Mashimba Ndaki kuja na majibu ya msingi yanayoonesha namna gani kama wizara wamejipanga kuhakikisha wananyanyua sekta ya Uvuvi nchini ili kuweza kuipatia Nchi mapato makubwa lakini pia kusaidia kupunguza changamoto ya ajira kupitia Uvuvi.
“Naomba niseme tu, hali ya Sangara katika Ziwa Victoria ni mbaya sana sasa sijui Wizara ya Mifugo na Uvuvi imeliona hili na kulitafutia ufumbuzi?. Nasema haya kwa kuwa Sangara ni bidhaa muhimu katika soko la samaki duniani,” amesema Ditopile na kuongeza:
“Viwanda villivyokuwepo mwaka 2014/2015 viliweza kuajiri vijana 12,000 katika sekta ya uvuvi, nasikitika kusema ajira imepungua kwa zaidi ya 50% na tuna vijana 4,000 tu wameajiriwa katika sekta ya uvuvi.”
More Stories
Rais Mwinyi aukataa msamaha wa Mzee Shamte
Majaliwa ammwagia manoti aliyekuwa mraibu dawa za kulevya
Butiku ataka nguvu ielekezwe kwenye maendeleo ya wananchi kuliko vyama