Friday , 19 April 2024
Home Kitengo Maisha Elimu Rais Samia afanya mapinduzi ya elimu Tabora, madarasa 74 yajengwa
ElimuHabari

Rais Samia afanya mapinduzi ya elimu Tabora, madarasa 74 yajengwa

Spread the love

IMEELEZWA kuwa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan, imefanya mapinduzi ya elimu kwa mkoa wa Tabora baada ya kufanikisha ujenzi wa madarasa 74 katika shule mbalimbali mkoani humo kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Kati ya madarasa hayo 74, 60 ni ya shule za sekondari na 14 ni ya vituo shinikizi. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Akizungumzia mapinduzi hayo mmoja Mkuu wa Shule ya Sekondari Kariakoo Leonard Nyasebwa ambayo ni miongoni mwa wanufaika amesema mapinduzi aliyoyafanya Rais Samia katika sekta ya elimu yamewagusa wananchi moja kwa moja.

Akizungumzia Shule anayoiongoza ya Kariakoo amesema uwiano wa wanafunzi katika vyumba vya madarasa unaopaswa kuwa wanafunzi 40 hadi 45 kwa darasa moja, katika shule hiyo uwiano wa awali ulikuwa wanafunzi 70 kwa darasa moja hali iliyokuwa ikiwatisha wanafunzi.

Hoja hiyo inaungwa mkono na Mwanafunzi Onjonisi Agustino ambaye amesema wakati anajiunga na shule hiyo alidhani atakuwa anaingia kwa awamu kama kaka zake walivyokuwa wakifanya.

“Walikuwa wanaingia saa moja hadi saa sita wanatoka na wengine wanaingia saa sita mpaka saa 12 jioni, lakini kwa sasa hatuna hilo tena.

“Sasa hivi madarasa ni makubwa, tunasoma kwa kuji-nafasi, upepo mzuri, tunasoma vizuri kwa furaha, tunamshukuru sana Rais Samia,” amesema.

Aidha kero za miundombinu katika shule hiyo pia ilihusisha matundu ya vyoo kwa wasichana lakini sasa Rais Samia ameleta suluhu.

Mwanafunzi Lucy Gerald amesema hapo awali walikuwa wanapata tabu hasa pale wasichana walipokuwa wanaingia katika siku zao za hedhi.

“Wengine walikuwa hawawezi kuendelea na masomo yao kwa sababu walikuwa hawana sehemu ya kwenda kujisitiri.

“Walikuwa wanaogopa kuendelea na masomo mengine darasani hivyo walikuwa wanaenda nyumbani na kukaa siku tatu hadi siku tano, lakini kwa sasa hali ni nzuri kwa sababu ujenzi wa vyoo umekamilika na wasichana wameendelea kuwa na uhuru, kujiamini na kuendelea na masomo yao,” amesema.

Aidha mmoja wa wanachi aliyezungumza na Mwandishi wetu, Hamis Said amesema wanamshukuru Rais Samia kwani madarasa hayo hawajawahi kuyaona tangu wamekua katika nchi hii.

“Kwa kweli ni mazuri na yanafurahisha na darsa haya hatukutozwa hata Shilingi 10. Hii serikali ya awamu ya sita, ninaweza kusema ndio serikali ya wanyonge.

“Kwa hiyo tunashukuru sana kwa hilo, nampa ‘Big up’ sana kwa kweli… Mama anafaa maana sina wasiwasi na uongozi wake,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

ElimuHabari za Siasa

Walimu 52,551 kupandishwa madaraja mwaka huu

Spread the loveNaibu Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala...

BiasharaElimu

NMB yatoa vifaa vya ujenzi kwa shule sita Nyasa  

Spread the loveBENKI ya NMB imetoa msaada wa vifaa mbalimbali vya ujenzi...

ElimuHabari Mchanganyiko

GGML yawapa mbinu wanafunzi Geita Boys kufikia malengo ya kitaaluma

Spread the loveKampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) imetoa mafunzo maalumu...

ElimuHabari Mchanganyiko

Wanawake GGML wawanoa wanafunzi Kalangalala Sec. kujitambua

Spread the loveKATIKA kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani, Umoja wa...

error: Content is protected !!