Sunday , 5 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa ACT-Wazalendo yajivunia mambo manne 2023
Habari za Siasa

ACT-Wazalendo yajivunia mambo manne 2023

Ado Shaibu
Spread the love

CHAMA cha ACT-Wazalendo, kimetaja mambo manne kilichofanikiwa kuyafanya ndani ya mwaka 2023 unaolekea ukingoni, huku kikitaja mikakati yake mipya kuelekea 2024. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Hayo yamebainishwa leo tarehe 29 Disemba 2023 na Katibu Mkuu wa ACT-Wazalendo, akizungumza na MwanaHALISI Online kuhusu mambo ambayo chama chake kimeyatekeleza ndani ya mwaka huu.


Mambo manne yaliyotajwa na Ado ni, kufanikiwa kusajili wanachama wake kidigitali, ACT-Wazalendo kufanikiwa kuwafikia wananchi wa majimbo yote 264 ya Bara na Zanzibar, wasemaji wake wa kisekta kuwa vinara katika kueleza matatizo ya wananchi, pamoja na kuibua viongozi wapya vijana.

“Tuwe wa kweli chama hiki ni kipya na kichanga kuliko vyama vingine kuna maeneo tulikuwa hatujawahi kufika lakini mwaka huu tumefika kwenye majimbo yote kupitia ofisi yangu tumepeleka maafisa waandamizi kwa ajili ya kuhakikisha kila jimbo linapata viongozi,” amesema Ado.

Mwanasiasa huyo amesema, kuelekea 2024, ACT-Wazalendo kimejipanga kujiimarisha Tanzania Bara ili kuwa na ngome nyingi zitakazowasaidia kushinda chaguzi na kupata wafuasi wengi, hususan ukanda wa Kaskazini.

Ado amesema ACT-Wazalendo kitaendelea kujiimarisha ili kipate matokeo mazuri kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2025 na Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa 2024.

“Mtu akifanya tathmini na uchambuzi atakubaliana na mimi kwamba ACT-Wazalendo imeimarika 2023, imejiwekea nafasi ya chama kinachokuwa kwa kasi na ni imani yangu kwamba uchaguzi wa 2025 utakaotanguliwa na uchaguzi wa serikali za mitaa ACT-Wazalendo itachora ramani mpya yta siasa za Tanzania. Itapata viongozi wengi kuanzia ngazi ya mtaa, udiwani, ubunge hadi urais,” amesema Ado.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Mbatia ambwaga Selasini, mahakama yaamuru alipwe fidia

Spread the loveMAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, imemuamuru...

Habari za SiasaTangulizi

Mkulo afariki dunia, kuzikwa kesho Kilosa

Spread the loveALIYEKUWA Waziri wa Fedha na Mbunge wa Kilosa (CCM), Mustafa...

Habari za SiasaTangulizi

Sabaya afutiwa kesi, ruksa kugombea uongozi

Spread the loveMwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali DPP leo Ijumaa amefuta rufaa...

Habari za Siasa

Serikali yasaka bilioni 3 kujenga daraja Mto Mpiji

Spread the loveSerikali imesema inaendelea na juhudi za kutafuta fedha kiasi cha...

error: Content is protected !!