June 30, 2022

Uhuru hauna Mipaka

ACT-Wazalendo watoa neno kujiuzulu Mbunge wa CCM

Juma Duni Haji

Spread the love

 

CHAMA cha ACT-Wazalendo, kimesema kinasubiri taarifa rasmi kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), kuhusu kujiuzulu kwa Mbunge mteule wa Konde, visiwani Pemba, kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Sheha Mpemba Faki. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Taarifa hiyo imetolewa jana tarehe 2 Agosti 2021 na Makamu Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo Zanzibar, Juma Duni Haji.

“ACT Wazalendo kimeona taarifa ya CCM, kupitia mitandao ya kijamii, kuhusu kujiuzulu kwa Mbunge mteule wa CCM, Sheha Mpemba Faki wa Jimbo la Konde- Pemba. Chama kinafuatilia kwa karibu kuhusu taarifa hii, ikiwemo kusubiri kupokea taarifa rasmi toka NEC),” ilisema taarifa ya Duni.

Aidha, Taarifa ya Duni ilisema Kamati Kuu ya ACT-Wazalendo, itafanya kikao cha dharura, mwishoni mwa wiki hii, kwa ajili ya kutoa msimamo wake kuhusu suala hilo.

“Chama kitatoa taarifa kamili ya msimamo wake kuhusu suala hili, baada ya kikao cha dharura cha Kamati Kuu kinachotegemewa kuketi wakati wowote mwishoni wa wiki hii,” ilisema taariufa ya Duni.

Awali, ACT-Wazalendo kilipinga matokeo ya uchaguzi mdogo yaliyompa ushindi Faki kupitia CCM, kwa madai kwamba mchakato wake haukuwa huru na wa haki. Hata hivyo, chama hicho tawala kilipinga madai ya kupora ushindi wa jimbo hilo.

Ushindi huo wa CCM, ulikifanya ACT-Wazalendo kipoteze jimbo la Konde, lililokuwa chini ya mwanachama wake Khatib Said Haji, aliyefariki dunia tarehe 20 Mei 2021, katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Uchaguzi huo mdogo uliofanyika tarehe 18 Julai 2021, uliitishwa na NEC kufuatia kifo cha mwanasiasa huyo. ACT-Wazalendo kilimteua Mohammed Said Issa, kulitetea jimbo hilo.

Taarifa ya Faki kujiuzulu ubunge, ilitolewa jana na Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM, Shaka Hamdu Shaka.

Kwa mujibu wa taarifa ya Shaka, Faki ameamua kujiuzulu wadhifa huo kutokana na changamoto za kifamilia.

error: Content is protected !!