May 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

TBC yaingia mkataba mnono na TFF

Spread the love

 

SHIRIKA la Utangazaji Tanzania (TBC) limeingia mkataba wa miaka 10, wa matangazo ya matnagazo ya Radio kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF). Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Mkataba huo una thamani ya Sh. 3.54 bilioni, na ulisaini hii leo jijini Dar es Salaam, ambao upande wa TFF, uliwakiliasha na Rais wa Shirikisho hilo, Wallace Karia, huku TBC ikiwakilishwa na Mratibu wa Miradi na Masoko wa TBC, Gabriel Ndelumaki kwa niaba ya Mkurugezni Mkuu.

Akitoa neno kwenye hafla hiyo Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa TBC, Gabriel Ndelumaki alisema kuwa wamechukua dhamani hiyo kwa kuwa wana uweledi na vifaa vya kutosha katika kurusha matangazo ya moja kwa moja.

“Tuna uweledi pamoja na vifaa vya kutosha katika kurusha matangazo ya moja kwa moja.

“Matangazo ya michezo yanawafikia wengi ndani na nje ya nchi, kwa kuwa TBC ina mtandao mpana kwa hivyo kuwafikia watu wengi,” alisema Gabriel.

Tukio hilo la leo ni la kwanza kwa TFF, kuingia mkataba wa urushaji wa matangazo ya Radio katika historia ya Ligi Kuu Tanzania Bara.

Kwa upande wa Rais wa TFF, Karia alisema kuwa fedha hizo zilizopatikana kwenye mkataba huo, zitakuwa na mgao sawa kwa wahusika wote.

“Hela hii ambayo imepatikana tutaigawa kwenye klabu na tutaigawa sawasawa kwa wahusika wote bila kuangalia ukubwa wa klabu,” alisema Karia.

Aliongezea kuwa kila klabu mara baada ya kupata mgao huo, zitatakiwa kuwasilisha hesabu za matumizi mara baada ya kukamilika kwa msimu na ambazo zimefanyiwa ukaguzi kwa mujibu masharti ya leseni ya klabu.

Akiongelea juu ya urefu wa makataba huo, katika kipindi cha miaka 10, Karia alisema kuwa huwezi kumpa mtu mkataba wa miaka mitatu, kutokana na uwekezaji aliofanya.

error: Content is protected !!