Sunday , 5 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa ACT-Wazalendo: Madeni ya Serikali yameifilisi NHIF
Habari za Siasa

ACT-Wazalendo: Madeni ya Serikali yameifilisi NHIF

Spread the love

MSEMAJI wa sekta ya uwekezaji, mashirika ya umma na hifadhi ya jamii wa ACT wazalendo, Mwanaisha Mndeme, amesema kuanzia mwaka 2018 hadi 2022 Shirika la Taifa la Bima ya Afya (NHIF) limejiendesha kwa hasara kutokana na madeni yaliyokopwa na Serikali. Anaripoti Apaikunda Mosha TUDARCo … (endelea).

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatano ya tarehe 31, Agosti 2022, katika ofisi ya chama hicho amesema mfuko wa bima umekuwa ukileta vifurushi vipya, kuwatoza wananchi gharama zaidi na kupunguza mafao wanayopata wananchi ili kufidia makosa yake na mkusisitiza kuwa wananchi hawapaswi kulipa gharama kwa maamuzi mabovu ya Serikali.

Mndeme amesema kufuatia ripoti ya mkaguzi na mthibiti wa hesabu za serikali (CAG) mfuko huo umepata hasara ya Sh. 1.5 billion kutokana na ukusanya hafifu wa madeni, utoaji wa mikopo na uwekezaji mbovu wa fedha za umma.

Aidha, ameitaka serikali kupitia wizara ya fedha ihakikishe mikopo yote inayodaiwa kupitia mashirika ya umma na wizara kurudishwa haraka ili kuupa uwezo mfuko wa taifa wa bima ya afya kujiendesha wenyewe na kusaidia kila mtanzania kupata huduma bora ya afya.

Aidha, ameeleza kuwa 85% ya nguvu ya watanzania hawapo katika mfumo wa bima ya afya na ameitaka serikali kuhakikisha mifuko ya hifadhi ya jamii inaunganishwa na huduma ya afya ili kuhakikisha kuwa kila mtanzania anaweza kupata huduma ya afya.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Mbatia ambwaga Selasini, mahakama yaamuru alipwe fidia

Spread the loveMAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, imemuamuru...

Habari za SiasaTangulizi

Mkulo afariki dunia, kuzikwa kesho Kilosa

Spread the loveALIYEKUWA Waziri wa Fedha na Mbunge wa Kilosa (CCM), Mustafa...

Habari za SiasaTangulizi

Sabaya afutiwa kesi, ruksa kugombea uongozi

Spread the loveMwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali DPP leo Ijumaa amefuta rufaa...

Habari za Siasa

Serikali yasaka bilioni 3 kujenga daraja Mto Mpiji

Spread the loveSerikali imesema inaendelea na juhudi za kutafuta fedha kiasi cha...

error: Content is protected !!