Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko ACT waivaa LATRA CCC nauli kupanda, wataka ivunjwe
Habari Mchanganyiko

ACT waivaa LATRA CCC nauli kupanda, wataka ivunjwe

Spread the love

CHAMA cha ACT Wazalendo kimeitaka Serikali kulivunja Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Usafiri Ardhini (Latra CCC) kwa kushindwa kusimamia vema masilahi ya walaji. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Akizungumza jana tarehe 16 Januari 2024 na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Mkoa wa Manyara wa chama hicho, Makamu Mwenyekiti, ACT Wazalendo Bara, Dorothy Semu amesema kuwa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Ardhini (Latra) imeongeza nauli bila kutathmini hali ya maisha ya wananchi.

Amesema nalo Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Usafiri Ardhini (LATRA CCC) limeshindwa kutekeleza wajibu wake katika kuchukua hatua hizo.

“Nauli zimepanda hata hapa Manyara nimeambiwa kutoka Babati Mjini kwenda Kiteto nauli imetoka Sh 15,000 hadi Sh 20,000, Babati Mjini kwenda Babati Vijijini ilikuwa Sh 1,000 mpaka Sh 3,000, Simanjiro kwenda Babati zamani ilikuwa Sh 18,000 sasa hivi Sh 23,000.” alisema Dorothy.

Dorothy alisema wakati hayo yote yanaendelea LATRA CCC lilitakiwa kutekeleza wajibu wake kwa kutoa tathmini ya hali ya wananchi na kushauri.

“Hili baraza linawajibu wa kuwalinda abiria lakini halijafanya kazi yake ambapo ni wazi nauli hizi zimewaelemea wananchi tusema baraza hili livunjwe na liundwe baraza ambalo itamlinda mwananchi,” alisema Dorothy.

Alisema kwa LATRA CCC imeshindwa kutekeleza jukumu lake la msingi sasa inatakiwa kuvunjwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari Mchanganyiko

Chongolo aonya viongozi vijiji kutouza NIDA kwa wageni

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amewaonya viongozi wa...

error: Content is protected !!