Thursday , 2 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Kipindupindu champonza bibi afya, RC atoa maagizo
Habari Mchanganyiko

Kipindupindu champonza bibi afya, RC atoa maagizo

Spread the love

MKUU wa mkoa wa Songwe, Dk. Fransisi Michael amemuagiza Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Mbozi, Abdallah Nandonde kumhamisha kituo cha kazi bibi afya wa mamlaka ya mji wa Mlowo wilayani humo, Anjela Kiwale kwa kushindwa kushindwa kuwajibika na kusababisha hatari ya mlipouko wa magonjwa ya kuhara. Anaripoti Ibrahim Yassin, Songwe…(endelea).

Dk. Michael ametoa maagizo hayo leo Jumanne alipofanya ziara ya kushtukiza katika Soko Kuu la Mlowo na lundo la taka katika dampo zilizozagaa katika biashara za watu huku maji machafu yakitiririka katika maeneo ya baba lishe na mama lishe.

Mkuu wa mkoa wa Songwe, Dk. Fransis Michael (aliyevaa kofia) akizungumza namna alivyosikitishwa na hali ya mrundikano wa taka ngumu katika soko la Mlowo wilayani Mbozi.

Amesema soko la Mlowo linawafanyabiashara wengi huku dampo lililopo likionekana wazi kuwa limezidiwa na taka nyingi ambazo zinakaa muda mrefu pasipo kuondolewa.

Amesema taka hizo zimekuwa kero kubwa wananchi hasa wafanyabiashara ambapo mvua zinaponyesha maji taka yanaingia kwenye biashara zao.

”Nimepewa taarifa hizi na wasamaria wema na nimefika hapa hali ilipo hifahi, hii inaonesha watumishi idara ya afya ni wazembe, bibi afya wa eneo hili hautoshi lazima aje mtu mwngine afanye kazi hapa wewe uende kwingine’,” amesema Dk. Michael.

Mwenyekiti wa mtaa wa Mlowo, Lucas Chitindi amesema hali ya uchafu katika soko hilo ni kero kubwa kwao na kwamba hukaa muda mrefu pasipo kutolewa hali inayohatarisha wananchi kupata magonjwa ya milipuko ikiwemo kipindupindu.

Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Mbozi, Abdallah Nandonde licha ya kuyapokea maagizo yaliyotolewa,  alieleza tatizo la taka kutoondolewa haraka inatokana na ukosefu wa magari kwani lipo moja pekee.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari Mchanganyiko

Chongolo aonya viongozi vijiji kutouza NIDA kwa wageni

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amewaonya viongozi wa...

error: Content is protected !!