Thursday , 9 May 2024
Home Kitengo Maisha Afya Wanavijiji wajenga zahanati kukwepa umbali mrefu kupata huduma
AfyaHabari Mchanganyiko

Wanavijiji wajenga zahanati kukwepa umbali mrefu kupata huduma

Spread the love

WANAVIJIJI wa Kata ya  Musanja Jimbo la Musoma Vijijini, mkoani Mara, wameamua kuanza ujenzi wa zahanati kwa nguvu zao, ili kukwepa adha ya kufuata huduma ya afya umbali mrefu. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mara…(endelea).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa hivi karibuni na Ofisi ya Mbunge wa Musoma Vijijini, Prof. Sospeter Muhongo, wanavijiji hao hulazimika kutembea umbali wa kilomita 10 kwenda kupata huduma za afya kwenye Kata jirani ya Murangi.

“Kata ya Musanja yenye vijiji vitatu haina Kituo cha afya wala zahanati hata moja katika vijiji vyake, hii ndio Kata pekee jimboni kwetu yenye hali kama hiyo. Mbunge ameendesha harambee ya ujenzi wa zahanati ya Kijiji cha Mabuimerafuru,” imesema taarifa hiyo.

Kupitia harambee iliyoongozwa na Prof. Muhongo, fedha kiasi cha Sh. 1,350,000 zilikusanywa, mifuko ya saruji 59 na kondoo mbili.

Prof. Muhongo alichangia mifuko 200 ya saruji, ambapo kamati ya ujenzi iliundwa.

Katika hatua nyingine, taarifa hiyo imesema zahanati ya Kijiji cha Nyabaengere, inakaribia kuanza kutoka huduma na kwamba maombi yakufungiwa umeme yamepelekwa TANESCO.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kimbunga Hidaya chaua 5, kaya 7,027 zikikosa makazi

Spread the loveSERIKALI imetoa tathmini ya athari za kimbunga Hidaya, kilichotokea tarehe...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafugaji kuku Ihemi wanufaika na mafunzo

Spread the loveWADAU  wa mnyororo wa thamani katika sekta ndogo ya kuku...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Serikali yaainisha mpango wa kusaidia wachimbaji wadogo

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameainisha mpango wa Serikali wa...

Habari Mchanganyiko

DAWASA yatekeleza agizo la Samia kwa kutangaza zabuni kielektroniki

Spread the loveKiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Godfrey Mnzava...

error: Content is protected !!