Thursday , 9 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Polisi waendelea kuwabana wanavunja sheria, operesheni 3D yaendelea
Habari Mchanganyiko

Polisi waendelea kuwabana wanavunja sheria, operesheni 3D yaendelea

Spread the love

 

JESHI la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Kimeendelea na operesheni ya kutoa elimu na kuwakamata wale wote wanaoendelea kuvunja sheria za usalama Barabarani huku Jeshi hilo likiwapongeza wale wote waliotii agizo la serikali la kuondoa namba ambazo hazijasibitishwa na mamlaka ya viwango Tanzania (TBS). Anaripoti bel Paul, Jeshi la Polisi Arusha … (endelea).

Akiwa katika Operesheni hiyo leo tarehe 19 Machi, 2024 Mkoani Arusha, Mkuu wa Operesheni za kikosi cha Usalama barabarani nchini kamishna msaidizi wa Polisi ACP, Nasoro Sisiwayah amesema kikosi hicho kinaendelea kuwakamata wale wote walio kaidi agizo la kuondoa namba zenye ujazo 3D na ving’ora.

ACP Sisiwayah ameongeza kuwa operesheni hiyo imelenga pia kukamata madeni ya wale wote waliofanya makosa barabarani na kupigwa faini ambapo amebainisha kuwa zoezi hilo linaendela nchi nzima huku akiwaomba watumiaji wa vyombo vya moto ambao wanadaiwa kuhakikisha wanalipa madeni yao kwa wakati.

Aidha amesema kuwa operesheni hiyo pia imehusisha kuwakamata wale wote wanaoendesha mwendo kasi vyombo vya moto ambapo amebainisha kuwa uchunguzi wa Jeshi hilo unapofanyika umebaini kuwa chanzo cha ajali nyingi ni mwendo kasi hivyo nao watakamatwa.

Nao baadhi ya madereva licha ya kupongeza operesheni hiyo wamebainisha kuwa undoshaji wa namba hizo utasaidia katika swala la ulinzi na usalama huku wakiliomba Jeshi la Polisi kikosi cha usalama barabarani kuendelea na operesheni hiyo ambayo itasaidia katika usalama.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Serikali yapunguza kodi ya makampuni kwa 20%

Spread the loveSERIKALI imepunguza kodi ya makampuni kwa asilimia 20, kutoka asilimia...

Habari Mchanganyiko

Mradi uliotaka kumng’oa madarakani Dk. Mpango waanza majaribio

Spread the loveMRADI wa maji wa Mwanga-Same-Korogwe, ambao Makamu wa Rais, Dk....

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Madiwani Msalala wampa tano DED kwa kuongeza mapato

Spread the loveMKURUGENZI wa Halmashauri ya Wilaya ya Msalala, mkoani Shinyanga, Khamis...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kimbunga Hidaya chaua 5, kaya 7,027 zikikosa makazi

Spread the loveSERIKALI imetoa tathmini ya athari za kimbunga Hidaya, kilichotokea tarehe...

error: Content is protected !!