Thursday , 9 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Polisi: Tumemkamata Mwabukusi, Mdude kwa mahojiano
Habari MchanganyikoTangulizi

Polisi: Tumemkamata Mwabukusi, Mdude kwa mahojiano

Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania, David Misime
Spread the love

Jeshi la Polisi nchini limethibitisha kuwakamata Wakili Boniface Mwabukusi na Mpaluka Said Nyagali maarufu kama Mdude kwa tuhuma za kutoa maneno ya uchochezi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dra es Salaam … (endelea).

Taarifa iliyotolewa leo Jumamosi na Msemaji wa Jeshi la Polisi, SACP -David Misime imesema wawili hao wamekatwa kwa mahojiano ambayo yanaendelea.

“Jeshi la Polisi kama lilivyo eleza jana tarehe 11 Agosti 2023 linawafuatilia ili liwakamate watuhumiwa walioandaa na kutoa maneno ya uchochezi, kazi hiyo inaendelea kufanyika kwa mujibu wa sheria.

“Jeshi la Polisi lilifanikiwa kuwakamata maeneo ya Mikumi Mkoani Morogoro majira ya saa nane na nusu usiku tarehe 12 Agosti 2023,” imesema taarifa hiyo.

Hayo yamejiri baada mapema asubuhi leo MwanaHALISI Online kuripoti taarifa za kukamatwa Mwabukusi na Mdude ambazo pia zilienea katika vyanzo mbalimbali.

Mwabukusi alikuwa mmoja wa wanasheria waliofungua kesi ya kupinga mkataba uliofumgwa kati ya serikali na Dubai.

Kukamatwa kwa Mwabukusi  kumekuja muda mfupi baada ya Mkuu wa Jeshi la Polisi kuutangazia ulimwengu, kwamba “kuna njama za kumuangusha Rais wa Jamhuri, Dk. Samia Suluhu Hassan.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Serikali yapunguza kodi ya makampuni kwa 20%

Spread the loveSERIKALI imepunguza kodi ya makampuni kwa asilimia 20, kutoka asilimia...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu, Halima Mdee hapatoshi

Spread the loveVITA ya maneno kati ya Makamu Mwenyekiti wa Chama cha...

Habari Mchanganyiko

Mradi uliotaka kumng’oa madarakani Dk. Mpango waanza majaribio

Spread the loveMRADI wa maji wa Mwanga-Same-Korogwe, ambao Makamu wa Rais, Dk....

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Madiwani Msalala wampa tano DED kwa kuongeza mapato

Spread the loveMKURUGENZI wa Halmashauri ya Wilaya ya Msalala, mkoani Shinyanga, Khamis...

error: Content is protected !!