Mataifa ya Afrika ya Magharibi yamesitisha mkutano muhimu wa kijeshi juu ya mzozo wa Niger ikiwa ni siku moja baada ya kusema maazimio ya mkutano huo yangelituma kuandaa kikosi cha kumrejesha madarakani kiongozi wa nchi hiyo aliyepinduliwa, Mohamed Bazoum.
Wakuu wa majeshi ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Uchumi ya Afrika Magharibi (ECOWAS) walikuwa wakutane leo Jumamosi katika mji mkuu wa Ghana, Accra, lakini jioni ya jana Ijumaa kulitolewa tamko la kuuakhirisha mkutano huo kwa muda usiojulikana. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa…(endelea).
Vyanzo hivyo vilisema mkutano huo ulikuwa umeandaliwa ili kuwaeleza viongozi wa ECOWAS juu ya njia bora zaidi za kuunda na kutuma kikosi hicho cha dharura nchini Niger.
Bado ECOWAS haijafafanua kwa undani kuhusu kikosi hicho wala ratiba ya hatua zake, huku viongozi wake wakisisitiza kuwa bado wanataka suluhisho la amani.
Akhirisho la mkutano huo lilitangazwa wakati maelfu ya wananchi wa Niger wakikusanyika kuunga mkono jeshi lao mbele ya kituo kimoja cha jeshi la Ufaransa jana Ijumaa.
Mkoloni huyo wa zamani ana wanajeshi zaidi ya 1,500 wanaoshiriki kile kinachoitwa “vita dhidi ya makundi ya kigaidi” kwenye taifa hilo la Ukanda wa Sahel.
Tangu mwaka 1990, ECOWAS yenye wanachama 15 imewahi kuingilia kijeshi kwenye mataifa sita miongoni mwa wanachama wake nyakati za vita vya wenyewe kwa wenyewe, uasi ama mkwamo wa kisiasa.
Leave a comment