Thursday , 9 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Chadema yaijibu CCM mashambulizi dhidi ya Rais Samia
Habari za SiasaTangulizi

Chadema yaijibu CCM mashambulizi dhidi ya Rais Samia

Spread the love

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema maridhiano yanayofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan, hayatazuia kuikosoa Serikali yake katika mikutano ya hadhara. Anaripoti Mwandishi Wetu, Geita…(endelea).

Msimamo huo umetolewa leo tarehe 31 Julai 2023 na Makamu Mwenyekiti wa Chadema Bara, Tundu Lissu, katika mkutano wa hadhara wa chama hicho uliofanyika mkoani Geita.

Baada ya Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuituhumu Chadema kwamba wanatumia mikutano ya hadhara kutoa kauli za kejeli dhidi ya Rais Samia, licha ya mema aliyowafanyia ikiwemo kuwapa ruzuku na kuwatoa vifungoni wafuasi wake.

“Ukitufunga bure tutakusema, ukituachia tutakusema, ukiiba tutakusema, ukigawa nchi yetu tutakusema na tutakusema mchana kweupe. Sisi hatuhongeki kama mlifikiri mnatuachia kama hongo hiyo haipo,” amesema Lissu na kuongeza:

“Mlichofanya hamjatupa chochote ambacho sheria za Tanzania zinasema sio za kwetu, sheria inasema  kufanya mikutano ni halali hivyo hamkutupa fadhila mliondoa haram mliyoweka wenyewe. Kazi ya mikutano ni kueleza wananchio ubovu ulioko madarakani ndiyo kazi yetu, kutakuwa na haja gani kufanya mikutano kwenda kumsifu mama hata anapofanya mambo ya hovyo.”

Jana Jumapili, akizungumza katika mkutano wa hadhara mkoani Tabora, Kinana aliitaka Chadema isitumie vibaya fursa ya kufanya mikutano ya hadhara kutukatan, kudharau na kukejeli Serikali ya Rais Samia.

“Tumekaa nao tangu Mei 2022 mpaka kikao cha mwisho Juni 2023, hakuna ajenda hata moja imetoka kwa CCM kwenda mezani, zote zimetoka kwao na nyingi tumezifanyia kazi, walikuwa wanachama wao wana kesi nyingi zimetazamwa na nyingine zimefutwa, jamani yote haya hayafai? Hayastahili kushukuriwa? Hayastahili Rais kuheshimiwa?” Kinana alihoji.

Mwanasiasa huyo alisema “Tumefungua mikutano kuja kusemwa, kusakamwa na kudhalilishwa? tumetoa ruzuku waliyoomba kusafiria kupata fursa ya kwenda kutusema na kututukana? Hatusemi tunafanya hisani lakini tumekuwa waungwana.”

Kinana aliitaka Chadema kuwa waungwana kwa kufanya siasa zenye hoja badala ya kujenga hoja kwa dharau.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Serikali yapunguza kodi ya makampuni kwa 20%

Spread the loveSERIKALI imepunguza kodi ya makampuni kwa asilimia 20, kutoka asilimia...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu, Halima Mdee hapatoshi

Spread the loveVITA ya maneno kati ya Makamu Mwenyekiti wa Chama cha...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Madiwani Msalala wampa tano DED kwa kuongeza mapato

Spread the loveMKURUGENZI wa Halmashauri ya Wilaya ya Msalala, mkoani Shinyanga, Khamis...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kimbunga Hidaya chaua 5, kaya 7,027 zikikosa makazi

Spread the loveSERIKALI imetoa tathmini ya athari za kimbunga Hidaya, kilichotokea tarehe...

error: Content is protected !!