Friday , 10 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Sheikh Ponda ataka Bunge lisikwamishe hatua kwa vigogo walioguswa na CAG
Habari za Siasa

Sheikh Ponda ataka Bunge lisikwamishe hatua kwa vigogo walioguswa na CAG

Spread the love

 

KATIBU wa Shura ya Maimamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda, amemtaka Rais Samia Suluhu Hassan, aanze kuwashughulikia vigogo waliohusika na vitendo vya ubadhirifu wa fedha na mali za umma, vilivyoibuliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG). Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Akizungumza jijini Dar es Salaam, leo tarehe 22 Aprili 2023, Sheikh Ponda, amesema kuna baadhi ya hatua zinapaswa kuchukuliwa mara moja kabla yakusubiri maazimio ya Bunge yanayitarajiwa kutolewa Novemba mwaka huu.

“Katika tukio la ripoti ya CAG, tunamshauri Rais achukue hatua zaidi hasa kwa yale mambo ambayo hayahitaji kusubiri hatua za bunge. Kwa mfano suala la kuundwa kwa Tume Huru ya Kumchunguza aliyekuwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), hilini mamlaka ya Rais,” amesema Sheikh Ponda.

Shekhe Ponda Issa Ponda

Katika hatua nyingine, Sheikh Ponda amelitaka Bunge lisikawie kufanyia kazi ripoti hiyo ya CAG kwa mwaka wa fedha wa 2021/22.

“Tunashauri Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutochelewesha shughuli za Kamati za Bunge zinazohusika na Usimamizi wa Fedha za Umma ili wananchi waone kuwa wawakilishi wao wanafanyia kazi masuala mazito yanayowahusu,” amesema Sheikh Ponda.

Aidha, Sheikh Ponda ameshauri suala la maadili liwe ajenda kuu ya ujenzi wa taifa, huku akihimiza watendaji wa mamlaka za umma wapewe dhamana kwa kigezo kikuu cha maadili.

1 Comment

  • Ukweli ni ukweli ndaima..! Cag alichokitoa kifanyiwe kazi, tuone kipi kinaendelea

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Vijana UVCCM Kagera wataka mwenyekiti wao ajiuzulu

Spread the loveVIJANA wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kagera wamemtaka Mwenyekiti...

Habari za SiasaTangulizi

Mpina awavaa mawaziri wanaompelekea majungu Rais Samia

Spread the loveMBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina (CCM) amewataka baadhi ya mawaziri...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

THRDC, Wizara ya Katiba wajadili uanzishaji haki binadamu katika biashara

Spread the loveMTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), umefanya...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Sitta ang’ang’ana wanafunzi watibiwe bure, Serikali yagoma

Spread the loveMBUNGE wa Urambo, Margaret Sitta, ameishauri Serikali iweke utaratibu wanafunzi...

error: Content is protected !!