Wednesday , 8 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Samia ashuhudia utiaji saini mikata 26 ya trilioni 1.9
Habari Mchanganyiko

Samia ashuhudia utiaji saini mikata 26 ya trilioni 1.9

Spread the love

RAIS Samia Suluhu Hassan leo Jumanne ameshuhudia utiaji saini mikataba 26 yenye thamani ya Sh trilioni 1.9 ambayo itakwenda kuimarisha upatikanaji wa umeme kwenye mfumo wa gridi ya Taifa katika mikoa mbalimbali Tanzania Bara.

Awamu ya kwanza ya mradi huo unaotekelezwa kwa muda wa miaka minne katika muda wa mwaka mmoja utagharimu Sh bilioni 500. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Hatua hiyo imekuja baada ya wizara ya nishari kwa kushirikiana na Shirika la Umeme nchini (Tanesco) kufanya tathmini na ukaguzi kuhusu chanzo cha kukatika kwa umeme na kubaini kuwa kuna ongezeko la matumizi makubwa ya umeme.

Mbali na ongezeko hilo pia matumizi ya mitambo chakavu isiyotosheleza na isiyo na usanifu bora kuweza kukidhi mahitaji ya umeme na shughuli za kiuchumi, ndio chanzo cha tatizo hilo.

Akizungumza katika hafla ya utiaji saini mikataba hiyo Ikulu jijini Dar es Salaam, Rais Samia Suluhu Hassan amesema bado kuna kazi kubwa ya kufanya katika kufikisha umeme katika vitongoji vyote nchini hasa ikizingatiwa sasa ni asilimia 43.9 pekee ya vitongoji hivyo vimefikiwa na huduma ya umeme.

Akifafanua namna mchakato wa mradi huo wa gridi imara ulivyoanza, Rais Samia amesema awali Waziri wa Nishati, Januri Makamba alimpeleka bajeti ya Sh trilioni 11 na kumrudisha.

Amesema baada ya kuridhia marekebisho ambayo wizara iliyafanya kulingana na upatikanaji wa fedha, maboresho hayo ya gridi ya Taifa yanalenga kuboresha upatikanaji wa umeme kwenye migodi hasa ya wachimbaji wadogo, vituo vya afya pamoja na skimu za umwagiliaji ambazo zinahitaji umeme kusukuma maji kuelekea kwenye mashamba ya vijana wanaoshiriki mpango maalumu wa serikali kuimrisha kilimo biashara.

“Miradi hii itapeleka maeneo 336 ya uzalishaji mali nchini, itatusaidia kujenga uchumi kwani vitongoji 1522 vitapata umeme pamoja na vituo vya afya hasa ikizingatiwa nchi yetu ni kubwa lakini hatua kwa hatua tutamaliza mradi huu licha ya kwamba tunajua malalamiko yatakuwepo lakini tutakwenda hadi tumalize,” amesema.

Aidha, Samia ameonya kuwa ili miradi hiyo ifanyike kwa haraka kwa kuzingatia maamuzi ya haraka.

Ameonya wakandarasi waliokosa zabuni za utekelezaji wa miradi hiyo kutokwenda kukata rufaa kwa mujibu wa sheria kwani watachelewesha utekelezaji wa miradi kwa sababu anaamini wakandarasi waliopitishwa ndio wakandarasi stahiki.

Pia amezitaka taasisi husika kama vila Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) kutozuia miradi hiyo kufanyika kwa haraka.

“Niwaombe sana pimeni yanayoletwa kwenu, msiturudishe nyuma kwa sababu sheria inaruhusu kufanya hivyo ndani ya miezi mitatu, kama waliowapitisha wakandarasi hawa kwa kuchukua rushwa, mkandarasi akivurunda mimi na wao,” amesema.

Pia amezitaka taasisi za serikali zinazohusika na utoaji wa vibali vya ajira kwa ajili ya wafanyakazi wa miradi hiyo, zisiweke urasimu kama uliotokea kwenye Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ambayo ilitumia mwaka mzima kuomba vibali ilihali suala la ukusanyaji wa kodi ni muhimu.

Pamoja na kupongeza kwa watanzania kupata kandarasi kwenye miradi hiyo, amewaonya kutotafuna fedha na kuanza kugawa kazi kwa wengine ili kupunguza gharama za kazi.

Ameionya pia wizara ya fedha kuhakikisha inatoa fedha za malipo kwa wakati pindi mkandarasi anapokamilisha kazi yake badala ya kuwazungusha ili wakandarasi wazawa wakue.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC, SILABU waungana kufikisha elimu ya fedha majumbani

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeingia makubaliano ya ushirikiano...

AfyaHabari MchanganyikoMakala & Uchambuzi

Kisukari cha mimba ni nini?

Spread the loveKisukari cha mimba ni aina ya kisukari kinachotokea kwa baadhi...

Habari Mchanganyiko

Mafunzo kwa bodaboda 395 yamkuna Meya Dodoma

Spread the loveNAIBU Meya wa Jiji la Dodoma, Asma Karama amepongeza mafunzo...

Habari Mchanganyiko

Samia aagiza huduma za dharura maeneo yaliyoathiriwa na kimbunga Hidaya

Spread the love   RAIS wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Samia...

error: Content is protected !!