Wednesday , 29 March 2023
Home Kitengo Michezo Rais Samia kununua kila goli la Simba, Yanga kwa Mil 5
Michezo

Rais Samia kununua kila goli la Simba, Yanga kwa Mil 5

Spread the love

 

RAIS Samia Suluhu Hassan, ametangaza kununua kila goli litakalofungwa katika michezo ya kimataifa ya Simba na Yanga itakayochezwa mwishoni mwa wiki hii. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Simba wanaoshiriki Ligi ya Mabingwa Afrika, itashuka uwanjani Jumamosi ya tarehe 18 Februari, 2023 dhidi ya Raja Casablanca, wakati Yanga ambayo inashiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, itacheza na TP Mazembe ya DR Congo siku ya Jumapili zote katika Uwanja wa Benjamini Mkapa, Dar es Salaam.

Akizungunza Msemaji Mkuu wa Serikali, Greyson Msigwa, amesema Rais Samia amefikia uamuzi huo ikiwa sehemu ya kuwapa hamasa timu hizo ili zifanye vizuri katika michuano hiyo ya kimataifa.

 

“Kila bao litakalofungwa kwenye michezo ya kimataifa itakayopigwa mwisho wa Juma hili, ambapo Simba na Yanga zitashuka dimbani, Rais wa Jahmhuri wa Muungano wa Tanzania atanunua kila bao kwa Shilingi Milioni 5, kama motisha,” amesema Msigwa.

Msigwa amesema Rais Samia anathamini mchango wa klabu hiyo kimataifa hivyo anaamini kuwa motisha huyo itasaidia kuwasukuma wachezaji kufanya vizuri na kulitangaza taifa kwa ujumla.

Simba na Yanga ambazo zipo katika hatua ya makundi ya michuano hiyo zilipoteza michezo yao ya awali ambayo walicheza nje ya nchi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

TANROADS wawataka watumishi wazingatie michezo kazini

Spread the love  WAKALA wa barabara Tanzania (TANROADS) imesema michezo inapaswa kuzingatiwa...

Michezo

Yanga: Fedha za Rais Samia zinaleta ari kubwa

Spread the loveUONGOZI wa klabu ya Yanga, umesema fedha zinazotolewa na Rais...

Michezo

Simba Sc. yamvulia kofia Rais Samia, yamuahidi makubwa dhidi ya Horoya

Spread the loveWAKATI timu ya Simba ikiibuka na ushindi wa bao 3-0...

Michezo

Taasisi ya TKO na TFF yawapiga msasa makocha wa kike 54

Spread the love WAKATI Soka la wasichana likichipua kwa kasi Taasisi ya...

error: Content is protected !!